Habari za Punde

Timu ya Taifa ya Zanzibar Yawasili na Kupokelewa na Vifijo Bandari ya Zanzibar.

 Waziri wa Habari,Utamaduni, Utalii na Michezo Mhe. Said Ali Mbarouk, akiipokea timu ya taifa ya Zanzibar ilipowasili katika bandari ya Malindi Zanzibar ikitokea Nchi Kurdistan katika michuano ya kuwania kushiriki Kombe la Dunia kwa Nchi zisizo wanachama wa FIFA, imeshinda nafasi ya tatu, ilishirikisha Nchi Tisa sio Wanachama wa FIFA. 
 Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakipokelewa na Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezom na Viongozi wa ZFA na Wananchi  wapenzi wa Michezo.
 Makamu wa Rais wa ZFA Alhaj Haji Ameir, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Taifa wakiwasili bandari ya Zanzibar kwa boti ya Kilimanjaro 3.
Wachezaji wa timu ya Taifa wakiwasili bandari ya Zanzibar kwa boti ya Kilimanjaro 3.






 Wachezaji wakishangilia walipowasili katika viwanja wa hoteli ya bwawani kwa sherehe fupi ya kuwazawadia na kuwapa shukrani kwa ushindi waliopata.
 Waziri wa Habari Utamduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk, akikabidhiwa Ngao ya Ushindi wa Tatu na Nahodha wa timu ya Taifa ya Zanzibar Abdi Kassim, baada ya kushinda nafasi ya Tatu katika Michuano ya kuwania nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa Nchi zisizo Wanachama wa FIFA,yaliofanyika nchini Kurdistan.
 Mchezaji Bora wa Michuano hiyo Nadir Haroub, akimkabidhi Ngao ya Mchezaji bora wa michuano hiyo, Waziri Said Ali Mbarouk,  katika sherehe za kuipongeza timu hiyo na kuizawadika kila mchezaji shilingi 250,000/= ikiwa ni pongezi kwa Wachezaji kufanikiwa kufika hatua hiyo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk, akitowa nasaha zake kwa Wachezaji wa timu ya Taifa katika ukumbi mdogo wa hoteli ya bwawani kwa mapokezi na kujumuika katika chakula cha mchana na kuwakabidhi zawadi.  
 Mkuu wa msafari wa timu ya Taifa ya Zanzibar Makamum Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Khamis Abdalla Said, akitowa maelezo ya safari yao katika michuano hiyo iliomalizika mwishoni mwa wiki nchini Kurdistan 
 Nahodha wa timu ya Taifa ya Zanzibar Abdi Kassim, akitowa shukrani kwa Wizara ya Habari na ZFA, wakati wa kukabidhi Ngao ya Ushindi wa Tatu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo.


 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said  Ali Mbarouk, akimkabidhi fedha mmoja wa mchezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar Khamis Mcha, akikabidhiwa shilingi laki mbili na nusu ikiwa ni zawadi kila mchezaji.   

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk, akijumuika na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar katika chakula cha mchana alichowaandalia wachezaji hao kwa ushindi wao wa nafasi ya tatu.
 Kucha wa timu ya Taifa ya Zanzibar Hemed Moroco akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili Zanzibar, jinsi timu yao ilipofanikisha michuano hiyo na kuonesha mchezo safi na kuwa kivutio kwa wananchi wa Kurdistan kwa kuvutiwa na mchezo wa wachezaji wake. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.