Habari za Punde

Waziri wa Mawasiliano Ziarani Bandari ya Mkoani Pemba

Na Nafisa Madai  
Waziri wa Miundombinu na awasiliano Zanzibar Hamad Masoud Hamad amesema amelazimika kukutana na wafanyakazi kazi wa Shirika la Bandari ya Mkoani Pemba ili kuwasihi wasije wakafanya mgomo baridi kama waliotaka kufanya wafanyakazi wa shirika hilo makao makuu Unguja.
Waziri Masoud ameyasema hayo wakati alipokua na mazungumzo na wafanyakazi kazi wa Shirika la Bandari ya Mkoani Pemba ambapo alisema uchumi wa Zanzibar kwa asilimia kubwa unategemea shughuli za bandari kuingiza na kutoa bidhaa mbalimbali nchini.

Amewataka wafanya kazi wa shirika hilo kuwa wa wazi katika kikao hicho bila ya kuficha na kwamba kama kutakuwa na jambo linalozorotesha utendaji wao wanapaswa kuliweka wazi kabla ya kufikia hatua ya kugoma.
Alifahamisha kuwa kila mtu ana wajibu wa kudai haki yake lakini watafute njia zilizo halali na wataweza kusikilizwa lakini si kwa njia ya mgomo hali ambayo inaweza kuzipoteza kabisa haki zao.
“Simkatazi mtu kufanya kazi kwa maslah yake kwani kila mtu alivyo anajijua mwenyewe lakini ninachotaka mimi mtu awe na nidhamu na afuate mikataba ya ajira inasemaje'',alisema Wazir Hamad
Aidha alifahaamisha kuwa Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar ilipiga marufuku migomo ya aina yoyote miaka kadhaa iliyopita ambapo alisema Serikali haitomvumilia mfanyakazi atakaefanya mgomo au kuchochea mgomo wowote.
Hata hivyo alisema wizara inafahamu hali ngumu ya maisha kwa wafanyakazi wake lakini wanachopaswa kukifanya ni kustahamili huku wizara ikiwa ipo njiani kutatua matatizo yote yaliyokuwepo.
Sambamba na hilo Waziri Masoud amesema mambo makuu yaliyopewa kipaumbele na serikal ni pamoja na kuifanyia matengenezo makubwa bandari hiyo katikati ya mwaka ujao pamoja na ujenzi wa bandari kuu ya mpiga duru ya malindi ili ziweze kuwa za kimataifa.
Kabla ya kukutana na wafanyakazi hao waziri huyo ambae alifuatana na watendaji wakuu washirika hilo pamoja na wizara alifanya ziara katika bandari hiyo ya mkoani kwa kukagua sehemu ambayo iliyokuwa ukituama maji wakati wa mvua baada ya kufanyiwa matengenezo.
Wakati akikagua bandari hiyo Waziri huyo pia alishudia boti ya seebuss 1 ikiwa inafunga gati bandarini hapo na kushuhudia abiria wakishuka wakiwa katika hali ya furaha nakulazimika kuhesabu abiria mmojamomoja ambao waliokuwa wakishuka katika boti hiyo
Baada ya kupata idadi ya abiria hao waziri hamadi alilazimika kukutana na kaptain wa boti hiyo pamoja na inchaji wa ZMA kwa kuhakikisha idadi kama ipo sawa na ile aliyohesabu awali.
Ziara ya hiyo ya siku mbili pia aliweza kutembelea barabara ya Mgwagadu ambayo ipo katika hatua ya kifusi na pia kufanya mazungumzo na wafanyakazi wa shirika hilo katika bandari ya wete na kutembelea barabara za mcc.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.