Habari za Punde

Balozi Seif Afutari na Wazee na familia zao

Na Othman Khamis Ame

Harakati za kufutari pamoja miongoni mwa waumini wadini ya Kiislamu zimeanza kushika kasi katika maeneo mbali mbali hapa Nchini. 

Wazee wa Kituo cha kutunza Wazee kiliopo Welezo walibahatika kujumuika pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwemo pia baadhi ya Viongozi wa Serikali, Mkoa na Manispaa. 

Futari hiyo iliyounganisha pia baadhi ya familia ya Wazee hao wa Welezo imekuja kufuatia mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambao ni miongoni mwa nguzo tano za Kiislamu zinazompasa kila Muumini wa Dini hiyo kuwajibika kuitekeleza. 


Akitoa shukrani kwa niaba ya Wazee hao pamoja na Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Mkurugenzi Utumishi wa Wizara hiyo Ndugu Iddi Ramadhan Mapuri amesema kitendo hicho kimeleta faraja kwa Wazee hao. 

Nd. Iddi amesema utaratibu huo wa Viongozi wa ngazi za juu kujumuika pamoja na Jamii katika maeneo mbali mbali huleta mapenzi mashirikiano zaidi miongoni mwao. 

Aliomba utaratibu huo uendelezwe kwa faida ya kustawisha umoja wa waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wananchi walio wengi Nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.