Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein leo amefanya uteuzi wa viongozi mbali mbali katika taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar,Dk .Abulhamid Yahya Mzee, Dk Shein amemteuwa Ali Salim Mchenga kuwa Afisa Tawala Mkoa wa Kusini,Unguja. Dk Makame Ali Ussi kuwa Afisa Tawala Mkoa Kaskazini Unguja na Khamis Salim Mohd Shambi kuwa Afisa Tawala Mkoa Kaskazini Pemba.
Aidha DKT Shein amewateuwa Mohamed Abdulla Ahmed kuwa Afisa Tawala wa Wilaya Mjini,Unguja.Omar Abdulla Juma kuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Kati, Unguja na Juma Abdulla Hamad kuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.
Katika Ofisi ya Rais Fedha ,Uchumi na Mipango ya Maendeleo Dk Shein amewateuwa Abdi Khamis Faki kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar,Hafidh Ussi Haji kuwa Naibu Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar.Seif Shaaban Seif kuwa Kamishna wa Mitaji ya Umma. Mwita Mgeni Mwita kuwa Kamishna wa Bajeti.Dk Rahma Salim Mahfoudh kuwa Kamishna wa Ukuzaji Uchumi katika Tume ya Mipango ya Zanzibar na Bihindi Nassor Khatib kuwa Kamishna wa Fedha za Nje.
Wengine aliewateuwa katika Wizara ya Miundo Mbinu na Mawasiliano ni Capt Abdulla Juma Abdulla kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Bandari na Abdi Omar Maalim ambae ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini.
Halkadhalika Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein Amewateuwa wafuatao kutoka Wizara ya Biashara ,Viwanda na Masoko ambapoMwanahija Almas Ali kuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC. Suleiman Juma Jongo Naibu Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC. Abdulmalik M .Bakari kuwa Ofisa Mdhamini wa ZSTC, Pemba na Khatibu Mwadini Makame kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango la Zanzibar (Zanzibar Bureau of Standards)
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment