Habari za Punde

Salamu za Mkono Idd kutoka Zacadia - Canada


Kwa niaba ya wana-Diaspora wote wanaoishi nchini Canada, Kamati Tendaji ya Zanzibar – Canadian Diaspora Association (ZACADIA) inachukuwa fursa hii kutoa mkono wa Eid El-Fitr kwa Waislamu wote duniani.

Mola atujaalie swaumu zetu na dua zetu tulizokuwa tukizisoma katika mwezi mtukufu wa Ramadhani zikubaliwe. Pia, tunaomba Mola atufungulie milango ya kheri na atupe mioyo ya kuendeleza kufanya mema kila siku.

ZACADIA inakutakieni Waislamu nyote kila la kheri katika hii Eid!

Katibu

ZACADIA 

Toronto, Canada.

Source: zanzibarnikwetu.blogspot.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.