Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, imemaliza utata wa usajili wa beki wake wa kimataifa wa Kenya, Paschal Ochieng kutoka AFC Leopard ya Kenya na sasa ataichezea timu hiyo katika msimu mpya wa ligi.
Habari zilizonaswa kutoka ndani ya uongozi wa wekundu hao, zimesema kuwa, Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, chini ya Mwenyekiti wake, Zacharia Hans Poppe ilikutana na mabingwa wa zamani wa Kenya AFC Leopards, na kumaliza tofauti zao.
Leopard ilikuwa inadai Simba imemsajili Ochieng kinyume na utaratibu, kwani bado ana mkataba wa miezi sita na klabu yake hiyo.
Kwa sababu hiyo, hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC) ya beki huyo wa zamani wa Yanga, inatarajiwa kuwasili nchini kuanzia jana.
Ochieng ni miongoni mwa wachezaji watano wa kigeni watakaokuwemo kwenye kikosi cha Simba cha msimu ujao.
Wengine ni kiungo Mussa Mudde, ambaye hata hivyo inaelezwa anaweza kukatwa akasajiliwa Keita wa Mali, washambuliaji Felix Sunzu kutoka Zambia, Emmanuel Okwi wa Uganda na Daniel Akuffo kutoka Ghana.
Tayari orodha ya wachezaji wa Simba waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom, imewasilishwa katka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa ajili ya uhakiki kabla ya kupitishwa.
No comments:
Post a Comment