Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed
Shein amemteuwa Fatma Kingwaba Hassan kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Huduma za Maktaba,Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi Dkt Abdulhamid Yahya Mzee amesema kuwa Uteuzi huo
wa Rais amefanya kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 3(2)(a)
cha Sheria ya Bodi ya Huduma za Maktaba,Zanzibar namba 7 ya mwaka
1993.
Uteuzi huo umeanza leo ijumaa tarehe 14 Disemba,2012.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
14/12/2012
No comments:
Post a Comment