WACHEZAJI sita wa Zanzibar Heroes, wakiongozwa na Nadir Haroub wameitwa kuunda kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia.
Stars na Chipolopolo zitapambana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 22. Chipolopolo inajiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, mwakani nchini Afrika Kusini.
Tangu Kocha Kim Poulsen aichukue Stars kutoka kwa mtangulizi wake, Jan Poulsen Mei mwaka huu, hakuwahi kuwaita wachezaji hao na amefikia uamuzi huo baada ya kuridhika na kiwango chao kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika hivi karibuni Kampala, Uganda.
Stars na Chipolopolo zitapambana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 22. Chipolopolo inajiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, mwakani nchini Afrika Kusini.
Tangu Kocha Kim Poulsen aichukue Stars kutoka kwa mtangulizi wake, Jan Poulsen Mei mwaka huu, hakuwahi kuwaita wachezaji hao na amefikia uamuzi huo baada ya kuridhika na kiwango chao kwenye michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika hivi karibuni Kampala, Uganda.
Nyota hao wanaoichezea timu ya Taifa ya Zanzibar, waliiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo wakiifunga Stars kwa penalti katika mchezo wa kuwania nafasi hiyo.
Wachezaji sita walikuwa kwenye kikosi cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichokamata nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kampala, Uganda, Kipa Mwadini Ally (Azam), Nassoro Masoud Cholo ( Simba), Nadir Haroub 'Cannavaro' ( Yanga), Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis wote wa Azam.
Poulsen alisema kuitwa kwa wachezaji hao kunafuatia kiwango cha kuridhisha kwenye mashindano hayo yaliyomalizika hivi karibuni.
Nadir Haroub kwa kipindi sasa alikuwa ameachwa na Kocha Paulsen baada ya kushuka kiwango hivyo pongezi pekee zimwendee Cannavaro kwa kufanya bidii na kutovunjika moyo wakati alipoachwa na kumwonesha Kocha kivitendo kitu gani anakikosa ikiwa hayumo katika timu ya taifa na si maneno.
Kilichonisikitisha katika uchaguzi wa wachezaji wa Timu ya Taifa ni kwamba wachezaji wote walioteuliwa ni wazanzibari lakini sasa wanacheza katika ligi kuu ya Tanzania bara. Hakuna hata mchezaji mmoja aliebahatika kuteuliwa ambaye anachezea ligi ya Zanzibar wakati karibuni tu Kocha Kim Paulsen alikuwepo Zanzibar kuja kuangalia vipaji katika ligi ya inayodhaminiwa na Grand Malt. Ninachojiuliza Kocha hakuona kifaa chochote kwenye ligi ya Zanzibar ambacho kinastahiki kuitwa katika timu ya Taifa ya Tanzania?
Katika miaka iliyopita tulikuwa na wachezaji tofauti waliokuwa wakiitwa katika timu Taifa wakicheza katika ligi kuu ya Zanzibar na walifanya vizuri tu kama kina Ali Bushiri ( Small Simba) , Zahor Salum ( Malindi), Abdulwakati Juma ( Small Simba), Innocent Haule ( Small Simba) , Juma Bakari Kidishi na Haji Mwinyi ( Mlandege), Hassan Mrisho Zitto ( KMKM) na kadhalika.
Hii ninaamini inaweza kuwaathiri kisaikolojia wachezaji wanaochezea ligi za Zanzibar kwamba hawatopata nafasi katika timu ya Taifa kama watachezea ligi za Zanzibar pekee ambapo tayari kuna masuala mengi yanasermwa kwamba tayari imekosa ushindani ( Competitiveness).
Pia itakuwa changamoto kwa wachezaji wetu wanaochezea Zanzibar kutafuta timu Bara kwasababu za kimaslahi na pia kuweza kuonekana kwenye medani hii ya soka na hivyo kutimiza ndoto zao na kwa maana nyengine ligi kuu ya Zanzibar itazidi kudorora.
Mfano mzuri Timu yetu ya Taifa ya Zanzibar iliyotuwakilisha Kampala utakuwa wachezaji takriban wote wanacheza katika ligi yenye ushindani ya Bara ambapo wachezaji wachache waliocheza Zanzibar unawehesabu kwa vidole. Hii ni timu yetu na sababu alizozisema Kocha Salum Bausi kuchagua timu hii ni kutokana na uzoefu ( experience) na muda mchache wa kuiandaa timu hivyo ukipata wachezaji wasioukuwa na uzoefu unaweza usifanye vizuri kwenye mashindano makubwa.
Kwa maoni yangu haya tunayoyaona yanaweza kuendeleza kuiua Soka la Zanzibar kwanza kwa kukosa ushindani, mapenzi ya timu, na sasa kukosa morali wachezaji kwa kutothaminiwa michango yao katika mchezo wa soka.
Safi sana..naskitika tu kwamba wamemuacha Suleiman kassim selembe'Fundi'..dogo anatisha!
ReplyDelete