Habari za Punde

Mji wa gesi wafurika

Na Mwandishi wetu

WAKATI sakata kuhusu gesi likiendele mkoani Mtwara, mvua kubwa iliyonyesha mkoani huo imesababisha mafuriko katika maeneo mbali mbali ya Mkoa huo huku wananchi wakianza kuzihama nyumba zao.

 Mvua hizo zimenyesha siku moja tu tokea wananchi wa Mkoa huo waandamane kuwafuata wafanyabiashara waliokaidi kufunga maduka yao ili kuhudhuria mkutano wa kupinga gesi kutoka Mtwara kupelekwa Dar es Salaam.


 Malalamiko hayo yalikuwa yanakabidhiwa kwa Wabunge wa Mkoa huo ambao ni Asnein Murji (CCM) na Said Baruani (CUF). 

 Mafuriko hayo yamesababisha mtafuruku mkubwa huku baadhi ya nyumba zikiwa zimefunikwa na maji ya mafuriko hasa katika eneo la chuo na mtaa wa Majengo.

 Wananchi wa maeneo hayo hawajui la kufanya baada ya mali na vifaa pamoja na nyumba kuharibika vibaya huku wengine wakiogelea kwenda kuokoa baadhi ya vitu vyao vilivyosalia kwenye nyumba. Taratibu za uokozi zinaendelea, ingawa zinakwamisha uchache wa vifaa vya kuokolea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.