Na Mwandishi maalum
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya TASAF kwa kipindi cha miaka mitatu.
Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema uteuzi huo umeanza Disemba 20, 2012.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Peniel M. Lyimo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TASAF.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni Dk. Khalid Salum Mohamed (Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar), Amran Masoud Amran (Afisa Mdhamini,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Pemba) na January R.L. Kayumbe – Idara ya Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Wengine ni Winfrida Annajoyce Nshangeki (Mkurugenzi Idara ya Serikali za Mitaa, TAMISEMI), Nyancheghe Anna Konyo Nanai (Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu) na Ally Msaki Ahmed (Mkurugenzi Msaidizi Soko la Ajira, Wizara ya Kazi na Ajira).
Wajumbe wenginei ni Constansia Peter Gabuse (Mkurugenzi Msaidizi Jinsia, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto), Ened A. Munthali (Mratibu wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais, Ikulu), Mariam Ally (Mchumi Mkuu, Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii),Hussein Mativila (Mhandisi, Wizara ya Ujenzi), Jerome J.R. Buretta (Kamishna Msaidizi, Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Uchumi), Zuberi Samataba (Mkurugenzi, Elimu ya Msingi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi), na Abbass Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Mtu mmoja kukabidhiwa majukumu (vyeo) vingi, jee hakuna watu watu wengine na ufanisi utapatikana au ni kutafutiana ulaji tu?
ReplyDeleteHao si watendaji wa TASAF bali ni wasimamizi wa sera, uteuzi upo sahihi.
ReplyDelete