Na
Khamisuu Abdallah
KINAMAMA
wametakiwa kujiunga na uzazi wa mpango utakaowawezesha kuziendesha vizuri
familia zao na kuepusha na vifo vya mama
na watoto nchini.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi katika hospitali ya Rahaleo, Muuguzi wa huduma za
mama na watoto, Mwanakhamis Alawi Nguzo, alisema uzazi wa mpango katika familia
ndio nguzo kuu itakayosaidia makuzi bora ya mtoto na kumjengea afya mama.
Alisema
kuwa njia hiyo pia inasaidia kupata taifa lililokuwa bora na kupunguza hasara
kwa serikali ya kuagiza dawa mara kwa mara nje ya nchi kwa ajili ya kuhudumia
watoto na mama wanaopata matatizo kutokana na kuzaa papo kwa papo.
Aidha
alisema kinamama wengi wamekuwa na dhana potofu ya utumiaji wa kinga hiyo na
kusema kuwa zinaathiri kiafya jambo ambalo alisema si la kweli.
"Kinamama
wengi wamekuwa na dhana potofu ya kudanganyana kuwa utumiaji wa uzazi wa mpango
unaweza kuwaathiri kiafya hasa kupata kensa ya uzazi jambo ambalo sio kweli,"
alisema.
Akizitaja
changamoto zinazowakumba katika kazi yao
ya kuwasaidia akina mama wanaokwenda kujiunga na kinga hiyo ni pamoja na kutofuata
ushauri wanaopewa na daktari pamoja na kuchagua njia za vijiti ambazo hudumu
kwa muda wa miaka 3.
Aliwataka
kinamama kujiunga na uzazi wa mpango kwani ni njia salama kwa wanafamilia na
dawa hizo hazina matatizo yoyote.
No comments:
Post a Comment