Habari za Punde

Jaji Mkuu wa Kenya akutana na wajumbe wa tume ya Katiba

 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (kushoto) akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga nje ya ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume leo (Ijumaa Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga amekutana na Wajumbe wa Tume kubadilishana mawazo na uzoefu wake kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
 Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto) akimwonyesha nakala ya Kitabu Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) nje ya ofisi za Tume mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na wajumbe wa Tume baina yao uliofanyika katika ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa Feb. 15, 2013). Mhe. Mtungi amekutana na Wajumbe wa Tume kuzungumzia uzoefu wake kuhusu uandishi na utekelezaji wa Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba.
Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) akibadishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) na Mjumbe wa Tume, Dkt. Sengondo Mvungi nje ya ukumbi wa Tume Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume leo Ijumaa (Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga alikutana na Wajumbe ili kubadilishana mawazo na uzoefu katika uandishi wa Katiba Mpya

1 comment:

  1. Kwa hakika hapa kwa Mhw. Dk. Willy Mutunga watafaidi mengi kuhusu mabadiliko ya katiba kwani ana uzoefu katika vuguvugu la kuleta mageuzi nchini Kenya, amekuwa Mkurugenzi katika taasisi ya Haki za Binadam Kenya (Kenya Human Rights Commission) na pia katika waliotafutwa kuchukua nafasi ya Jaji Mkuu aliwashinda wengi katika mahojiano ya ana kwa ana na Tume ya Uajiri ya Mahkama nchini Kenya.

    Pia Tume imtafute Prof. Ahmed Idha Salim aliyekua mwanatume wa Tume ya kurekebisha Katiba Nchini Kenya na wanatume wenzie Mawakili maarufu Kenya Prof. PLO Lumumba na Ibrahim Lethome (Huyu upande wa Mahkama ya Kadhi) ambayo kwa sasa imewekwa lakini haina mfumo kisheria nchini. Yeye ana utaalamu kisheria ya Nchi pamoja na Kidini amesoma ana Shahada ya Uzamifu kutoka vyuo vya nje.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.