Habari za Punde

Siku ya Sheria ilivyoadhimishwa leo

 Kikundi cha Wasanii kutoka Mafunzo wakiburudisha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria zanzibar,ambapo kauli mbiu "Kutokomeza Unyanyasaji Kijinsia",katika uwanja wa Bustani ya Victoria Garden leo
 Baadhi ya Makadhi wa walioalikwa katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria,katika uwanja wa Bustani ya Victoria Garden,wakifuatilia kwa makini harakati za maadhimisho hayo
zilivyoendelea na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali
 Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria Zanzibar,sherehe zilizofanyika leo katika viwanja vya bustani ya Victoria garden Mjini Zanzibar,mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein
  Viongozi wa Dini mbali mbali na Majaji wa Mkoa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,aliyoitoa leo katika kilele
cha maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar,katika Uwanja wa bustani ya Victoria Garden
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) na Kaimu Waziri wa Katiba na Sheria pia Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui,alipowasili
katika viwanja vya Victoria Garden,katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar,zilizofanyika leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kushoto) Jaji Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Fakih Jundu,(kutoka kushoto) na Kaimu
Waziri wa Katiba na Sheria,pia Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui,(kutoka kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi khamis,Spika wa baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,wakiangalia Kikundi cha wasanii cha Black Roots kilipokua kikitumbuiza katika kilele cha Siku ya Sheria leo.
 Viongozi wakisimama wakati wimbo wa Taifa wa Zanzibar ukipigwa na Brass band kikosi cha polisi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar.mara alipowasili Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa ndio mgeni rasmi katika hafla hiyo,iliyofanyika viwanja vya Victoria garden Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akionesha jarida la Mahakama baada ya kulizindua wakati wa sherehe za maadhimisho ya kilele cha Siku ya
Sheria Zanzibar,zilizofanyika leo,katika viwanja vya Victoria garden Mjini Zanzibar,(kushoto), Kaimu Waziri wa Katiba na Sheria,pia Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui,na (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu
 Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Ibrahim Mzee,alipokuwa akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar,zilizofanyika leo,katika viwanja vya
Victoria garden Mjini Zanzibar,ambapo ujumbe wa mwaka huu unasema "Kutokomeza Unyanyasaji Kijinsia".[
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Wananchi na wanasheria wakati wa sherehe za maadhimisho ya kilele cha Siku ya Sheria
Zanzibar,zilizofanyika leo,katika viwanja vya Victoria garden Mjini Zanzibar,(kushoto), Kaimu Waziri wa Katiba na Sheria,pia Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui,na (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.

  [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

2 comments:

  1. sheria iko wapi nd rais , hebu waulize watu wanaokwenda kwenye hizo mahakama zetu huko znz na tanganyika hufanyiwa mambo gani? kama una pesa utainunua haki hata kama si yako , na kama hohe hahe basi hata kama ni haki yako utaipoteza , hakuna sheria wala wanasheria wote ni majambazi tu walivaa uniform au sare na kupewa leseni kuwaibia wananchi ,lakini sokwe na ngedere lao ni moja kwa hio sishangai serikali na mahakama kuwa ni kitu kimoja kwani hulindana maslahi yao ya kijambazi kwa wanyonge wasitambua lolote .........

    ReplyDelete
  2. upumbavu mtupu Zanzibar imekwisha hakuna tena dini wala nini Makadhi wazima ambao wanategemewa kusimamia masuala ya dini ya kiislam pamoja na waislam wamekaa wanatizama ngoma na watu wanavokata viuno, wakiambiwa ukweli waanze kuita watu Al qaida na Al shabaab.

    Allah hajalala.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.