Habari za Punde

Uzinduzi wa Maskani ya Mzee Idrisa Abdulwakili na Maadhimisho ya miaka 36 Nungwi leo

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, akisalimiana na Viongozi na WanaCCM wa Maskani ya mpya ya Mzee Idrisa Abdulwakil Sogea, alipowasili kwa ufunguzi wa maskani hiyo ikiwa ni shamrashamra za kutimia kwa miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, akikata utepe kuashiria kulifunguwa Jengo Jipya la Maskani ya Mzee Idrisa Abdul Wakili Sogea.ikiwa ni maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM na kutimiza miaka 36. 
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, akiwahutubia wanachama wa CCM wkati wa uzinduzi wa jengo la Maskani yao Sogea.
 Katibu Mwenezi wa CCM Jimbo la Magomeni Abdi Ali Mzee ( MROPE) akitowa maelezo wakati wa ufunguzi wa jengo la maskani ya CCM ya Mzee Idrisa Abdulwakil Sogea, ikiwa ni moja ya sherehe za kuadhimisha miaka 36 ya CCM.
 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakipita mbele ya mgeni Rasmin Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (hayuko pichani ) Mhe. Haji Omar Kheri. ikiwa ni maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa Chama cha Mapinduzi zilizofanyika katika viwanja vya Mpira Nungwi Zanzibar.
 Maandamano ya wapanda baskeli yakipita ikiwa ni maadhimisho ya sherehe za CCM.
 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishindano katika mchezo wa kuvuta kamba wakati wa maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM, zilizofanyika katika viwanja vya Nungwi Wilaya ya Kaskanizi A Unguja.

 
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Haji Omar Kheri, akiwahutubia Wanachama wa CCM katika viwanja vya mpira Nungwi ikiwa ni maadhimisho ya sherehe za Chama cha Mapinduzi kutimiza miaka 36 yaloaadhimishwa leo 3-2-2013. 
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe. Haji Omar Kheri, akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa CCM Mwanakhamis Bakari, wakati wa maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.
 Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi wakila Kiapo baada ya kukabidhiwa kadi zao na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Haji Omar Kheri.
 Vijana wa Kimasai wakitowa burudani wakati wa maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 36 yalioadhimisho Mkoa wa Kaskazini Unguja katika viwanja vya mpira Nungwi.
Vijana wa Sarakasi wakionesha umahiri wao wa mchezo huo wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 36 ya CCM Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.