Habari za Punde

Wavu Zanzibar yafanywa ngazi

 
Na Mwajuma Juma, Dar es Salaam
TIMU ya mpira wa wavu ya Magereza, imeendelea vyema na kampeni zake za kutetea ubingWa wa Muungano baada ya jana kuiadhibu Polisi Zanzibar seti 3-0.

Katika mchezo huo wa ufunguzi uliochezwa viunga vya uwanja wa Taifa Dar es Salaam chini ya ugeni rasmi wa Katibu wa TOC Filbert Bayi, kila timu iliingia uwanjani kwa ari na nguvu ya kusaka ushindi na hivyo kutoa burudani muwanana kwa watazamaji.

Licha ya kupoteza mchezo huo, Polisi ilionesha kiwango cha juu lakini ilikosa mbinu katika umaliziaji na kujikuta wakishindwa kuambulia angalau
seti.

Kulala kwa maafande hao, kumefanya timu tatu kati ya nne za Zanzibar kupoteza mechi kwa wanawake na wanaume, baada ya hapo juzi Nyuki wanaume kufungwa 3-0 na Magereza, huku akinadada wa Wete wakiangukia pua mbele ya maanti wa Jeshi Stars kwa idadi kama hiyo.

Katika mechi za mapema uwanjani hapo, Magereza ikaiadhiri JKT kwa kipigo cha seti 3-0, Mzinga ikaishinda Nyuki 3-0 ikiwa mechi ya pili kwa Nyuki kupoteza katika kundi B ambalo pia lina timu za Polisi, Magereza na Mzinga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.