Habari za Punde

Kesi ya Uamsho Zenji sasa kuendelea Dar

 
Na James Magai, Dar es Salaam.
 
Kesi ya uchochezi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya Zanzibar (Jumiki),Sheikh Faridi Hadi Ahmed (41), na wenzake 9, sasa imepangwa kuunguruma katika Mahakama ya Rufani Dar es Salaam, Juni 10, mwaka huu.
 
Sheikh Faridi na wenzake wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Zanzibar. Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mselem Ali Mselem, Mussa Juma, Azzan Khalid Hamdani, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan Bakari, Ghalib Hamada Juma, Abdallah Saidi na Fikirini Fikirini.
 
Washtakiwa hao kupitia kwa mawakili wao, wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Rufani Tanzania, wakiomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Zanzibar, dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, wa Machi 11, mwaka huu.
 
Mahakama hiyo, katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Abrahamu Mwampashi, ilitengua mwenendo wa maombi ya dhamana ya washtakiwa yaliyotolewa na na mawakili wao kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Oktoba 25, siku washtakiwa hao waliposomewa mashtaka.


Pia Mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi ya marejeo ya washtakiwa hao kuhusu uamuzi wa Msajili wa Mahakama Kuu kuwakatalia dhamana na kuamuru warejeshwe rumande hadi tarehe iliyopangwa kutajwa kwa kesi hiyo, pamoja na pingamizi la awali (PO) la upande wa mashtaka.
Katika maombi yao kwa Mahakama ya Rufani, washtakiwa hao wanaiomba Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa hiyo ya DPP, kwa madai kuwa hakuna rufaa iliyofunguliwa na mjibu maombi (DPP) dhidi ya uamuzi na amri ya Mahakama Kuu anayoipinga.
 
Washtakiwa hao wanabainisha kuwa taarifa ya kusudio la kukata rufaa iliyowasilishwa mahakamani hapo na mjibu maombi haihusiani na uamuzi huo wa Mahakama Kuu wa Machi 11, mwaka huu.
 
Wanafafanua kuwa uamuzi huo wa Mahakama Kuu wa Machi 11, mwaka huu hauwezi kupingwa kwa rufaa wala kwa maombi ya marejeo katika Mahakama ya Rufani
 
 Maombi haya yamepangwa kusikilizwa na jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, Juni 10, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
 
Jopo hilo la majaji watakaosikiliza maombi hayo linaongozwa na Jaji January Msiffe, akisaidiana na Jaji Salum Massati na Jaji William Mandia.
 
Maombi hayo yamewasilishwa chini ya hati ya dharura wakiomba mahakama iyasikilize mapema .
Dar es Salaam. Kesi ya uchochezi inayomkabili Kiongozi wa Jumuiya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu ya Zanzibar (Jumiki),Sheikh Faridi Hadi Ahmed (41), na wenzake 9, sasa imepangwa kuunguruma katika Mahakama ya Rufani Dar es Salaam, Juni 10, mwaka huu.
 
Sheikh Faridi na wenzake wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.
 
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mselem Ali Mselem, Mussa Juma, Azzan Khalid Hamdani, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan Bakari, Ghalib Hamada Juma, Abdallah Saidi na Fikirini Fikirini.
 
Washtakiwa hao kupitia kwa mawakili wao, wamewasilisha maombi katika Mahakama ya Rufani Tanzania, wakiomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Zanzibar, dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, wa Machi 11, mwaka huu.
 
Chanzo - Mwananchi

2 comments:

  1. Hawajamaa wao ndio wanao twambia,mwauchaka au hamuutaki leo hatujafika nusunjia wao wameona pahala pekee watakapo pata haki ni kwenye mahkama ya hao makafiri,watanganyika,sasa kama tumeuvunja mapema wangekimbilia wapi?. kukata rufaa?

    ReplyDelete
  2. "Baniani mbaya, kiatu chake dawa"...hawa ni watu wa kuwasamehe tu, hawajui walitendalo!

    Hata maalim seif, wakati wa siasa za 'kijahil'1995-2005 kimbilio lake kubwa lilikua hoteli ya STAR LIGHT(Tanganyika)

    Na sio yeye tu, bali WAzanzibari wengi walioonja siasa chafu za Komandoo waliishia huko!

    Al-marhum Dr. Omar Ali Juma aliwahi kuwatania akasema" Mwanya hapo hapo, mwakojoa hapo hapo, kisha walala hapo ahapoa"

    Allah awaongoze!!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.