Habari za Punde

Maalim Seif afungua kongamano la pili la kitaifa la maridhiano

 Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika ufunguzi wa kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
 Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika ufunguzi wa kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Mzee Hassan Nassor Moyo akizungumza katika kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
 Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Ismail Jussa Ladhu, akizungumza katika kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
 Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Hassan Nassor Moyo (kushoto) na Mjumbe wa kamati hiyo Ismail Jussa Ladhu, wakibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa kongamano la maridhiano lililofanyika hoteli ya bwawani.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la pili la maridhiano Zanzibar lililofanyika hoteli ya Bwawani, wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, katika ufunguzi wa kongamano hilo. (Picha, Salmin Said, OMKR)
 
Na Hassan Hamad, OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amesema dhamira ya msingi ya ukombozi wa Zanzibar kupitia Mapinduzi ya Januari 12, 1964, ni Zanzibar kuweza kujitawala yenyewe na kuwa na mamlaka kamili.
 
Maalim Seif ameeleza hayo katika ukumbi wa salama hoteli ya Bwawani, wakati akifungua kongamano la pili la kitaifa linalohusu Maridhiano ya Wazanzibari.
 
Amesema dhamira hiyo ya Mapinduzi ilianza kukiukwa baada ya kutiwa saini kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao uliipunguzia Zanzibar mamlaka yake.
 
Amesema wakati Wazanzibari wanapodai kuwa na mamlaka kamili wanatetea haki na maslahi ya nchi yao, na kwamba hakuna sababu ya kubezwa wala kupuuzwa.
Amefahamisha kuwa akiwa ni kiongozi wa Zanzibar, atasimamia na kutetea mawazo ya wazanzibari waliowengi katika kupata haki zao za msingi ndani na nje ya Zanzibar.
 
Akifafanua zaidi kuhusu msimamo wake amesema hiyo haina maana kuwa Wazanzibari hawataki Muungano, bali wanataka kuwepo kwa Tanzanyika na Zanzibar zenye mamlaka kamili, halafu kuwepo na muungano wa mkataba, ili kila nchi iweze kuendesha mambo yake kwa uhuru.


“Kuwa na mamlaka kamili sio kwa maslahi ya watu wachache bali kwa watu wote, ni kama mvua, yaani inaponyesha mimea yote inanawirika”, alifafanua Maalim Seif na kuongeza,
 
“Tunataka kurejesha heshima ya nchi yetu, tuwe na sera na Wizara yetu ya mambo ya nje, bendera yetu ipepee nchi za kigeni, Umoja wa Mataifa na Jumuiya nyengine za Kimataifa zikiwemo Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki”.
 
Amewataka wanakongamano hao kuwaongoza wajumbe wa mabaraza ya katiba katika kutetea maoni na maslahi ya Zanzibar.
 
Akizungumzia kuhusu mafanikio ya maridhiano amesema yamerejesha umoja wa wazanzibari na kuondosha uhasama na chuki miongoni kwa wananchi.
 
Ameipongeza kamati ya maridhiano chini ya Mwenyekiti wake Mzee Hassan Nassor Moyo kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuyaendeleza maridhiano hayo na umoja wa wazanzibari.
 
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ambaye ni mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo amesema maridhiano hayo yaliyoasisiwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar dkt. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, yameondoa fitna na chuki zilizodumu kwa muda mrefu miongoni mwa wananchi.
 
Amesema kamati yake inaisubiri kwa hamu kubwa rasimu ya Katiba mpya itakayotolewa, ili waweze kuichambua kuona kama imezingatia maoni ya wananchi na maslahi ya Zanzibar.
 
Akiwasilisha mapendekezo ya kamati hiyo Mzee Moyo amesema kila nchi katika Muungano inapaswa kuwa na uraia wake, sera yake ya mambo ya nje na Muungano uwe na JINA la “Muungano wa Jamhuri za Tanzania” au “United Republics of Tanzania”.

21 comments:

  1. ndugu yangu sharif nakupongee kwa kuwa mkweli lakini sisi hatutaki muungano wowote ule , hata mkataba hatutaki kwani humo pia kutakuwa na ujanja ujanja , bora kila mtu achukue nchi yake , tushirikiane tu kama vile tunavyoshirikiana na kenya uganda nk , ingawa ushirikiano wetu unaweza kuwa zaidi ya huo wa east africa , lakini mambo ya mikataba hatutaki kabisa kabisa

    ReplyDelete
  2. Usitusemee, sisi wengine tunauhitaji kama uhai. Tunajua kuwa bila Muungano ni gomvi tu hapa Zanzibar.

    ReplyDelete
  3. mtwara wameanza udini mbeya nani achinje kukatana mapanga kwa siasa zote hizi hutokea tanganyika

    ReplyDelete
  4. wazanzibar walikuwepo na tulikuwepo na tupo kabla ya tanganyika,watanganyka husema wazanzibar wakitoka nje ya muungano watagawana unguja na upemba,hizi ni hisia dhaifu za nyrere,tanganyika inakabiliwa na udini sababu wakristo wanawalemea waisilam na kuwadhulumu kupitia mfumo kristo,kuchinja nyama sensa hiini mifanohai,necta ,siasa chafuchaguzi za diwanitu wanachinjana na kukatana mapanga siasa chafu utekaji na kungowa watukucha ,mwangosi ,sikwambii mtwara hatanyinyi tanganyika haitokuwa salama zanzibar matokeo ya fujo na ubaguzi ni siasa za tanganyika kupitia ccm ukitaka kujuwa hili kuzamakwa spice ilender wazanzibar wa unguja na pemba walivyoguwsa na msiba lakini kuzama kwa skajit watu walikuwa wakisema wakati inatokea huko itakuwa watananyika wengi tu kuliko sisi wazanzibar watu kifo skajit hakikuhit sana

    ReplyDelete
  5. tunacho kidai sisi sio kuuvunja mungano bali ni muungano wausawa huku kila nchi ikiwa namamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa kisha tukashirikiana kwa makubaliano maalumya kiuchumi na kijamii

    ReplyDelete
  6. @ano 6.15 , si tatizo waitishe kura ya maoni tuone nani mkweli. Kwa kuongezea tu mapinduzi hayakuletwa ili wazanzibari wajitawale , isipokuwa ilikuwa ni njama ya mwl nyerere kutaka kuitawala zanzibar kwa njia ya muungano huo ndio ukweli na ndio maana mpaka leo ukizungumzia muungano inakuwa kama nongwa kwa watanganyika, lakini msisahau kuwa ndugu zetu pia watanganyika wanataka nchi yao iwe peke yao huu muungano ushawatosha hata wao.Wala si kweli kama bila muungano tutagombana hizi ni fitna zisizo na msingi zimepandikizwa na wachache wenye faida na muungano.@ ano 8.24 udini umeletwa na Mwl Nyerere ndie alipandikiza mbegu za udini , ukiangalia katika kila sekta zote muhimu iliwapa jamaa zake, na mpaka leo hii , angalia wizara zote , jeshi , polisi, akina tra , elimu, uhamiaji , kila mahali hata afya mfano mdogo angalia muhimbili bodi yake ina akina nani , waajiriwa wengi ni akina nani? wamebakia kuwadanganya kwa kupiga picha watu wanaovaa hijabu ktk sherehe mbalimbali ili waonekane kuwa kuna ka usawa , kuwapa ukubwa akina alhajat ktk sensa , akina mwema , akina jaji mkuu , akina bilali huu ni unafiki mtupu. Kama mwongo angalia hata kazi ambazo hazitaki akili nyingi kama za kukusanya parking fee hapa dar es salaam ni akina nani wamepewa kazi hizo? wakishasoma haya niliyoandika , watachofanya watawavalisha vihijabu baadhi yao ili waonekane kuna ka usawa . Uhuru wa zanzibar ni lazima upatikane kwa uwezo wa mola hakuna chenye mwanzo ila huwa na mwisho msisahau , umefika wakati uvunjwwe muungano kwa amani na upendo ili tubakie kushirikiana , kuliko kuvunjika kwa umwagaji damu na kuacha chuki na madhila.

    ReplyDelete
  7. nakushangaa sharifu hamadi vipi unasema wizara ya mambo ya nje tu , sisi wananchi wako tunataka kila wizara iwe peke yetu isiungane na chochote kile , labda wizara ya kilimo na afya . Wizara nyengine zote zisiwepo kwenye muungano , tuwe na kila kitu chetu wenyewe , kuanzia jeshi la wanachi , polisi, magereza , uhamiaji , elimu , usafiri , nishati , ardhi, mambo ya ndani, kwa kifupi hatutaki muungano kwenye lolote lile , tushirikiane tu katika nyanja zitazokubalika, msemaji hapo anonymus 8.45 ana mtazamo wa mbali maneno ya kuzingatia japokuwa Rais Nyerere amefariki lakini athari zake zinaonekana mpaka leo hii

    ReplyDelete
  8. Anonymous wa sita, tungependa sana kusoma maoni yako lakini kwa kweli tumeshindwa.

    Umejitahidi kutumia vituo lakini ukashindwa kuyagawa maoni yako ktk paragrafu na hili ni jambo muhimu sana ktk uandishi.

    Pointi tofauti huwekwa ktk paragrafu tofauti na wakati mwengine kama unashindwa kutambua pointi zako na habari yako ni ndefu, kila baada ya mistari mitatu/minne gonga 'enter' mara mbili.

    ReplyDelete
  9. "Kitulacho, ki nguoni mwetu"..tusafishe nyumba kwanza kabla ya kumshambulia jirani!

    ReplyDelete
  10. Maalim

    Nadhani haya makongamano hatuhitaji tena hasa hapa mjini, tumeshamka zamani, kila unachosema uwamsho washasema zamani, kama unataka kufanya makongamano tukakushauri fanya mkowa wa kusini, huko naona bado maji ya kijani yanawapelekesha, wanahitaji elimu kuelimishwa nini madhumuni ya muungano, na kwa nini tunahitaji zanzibar huru, tuache siasa.

    ReplyDelete
  11. Tumechoka na makongamano ya uchochezi sasa tunaomba makongamano ya kimaendeleo.

    ReplyDelete
  12. Mkoa wa Kusini hauna vifuu tundu. Hatuhitaji makongamano ya kinafiki kama haya. Tunayoyafanya tunajua kabla hata hiyo Pemba haijazaliwa. Sisi sio limbukeni wa madaraka wala urua wowote. Tunaelewa Muungano ndio mkombozi wa Zanzibar. Yakweli hamsemi mbona. Wezi wa ardhi zetu ni wabara? Ni sisi wenyewe. Maovu yote ya tindikali ni wabara? Ni sisi wenyewe. Rushwa kila pahala ni muungano? Wizi serikalini ni muungano? Siasa za unafiki basi. Muungano oyeeeeee!!!!!!

    ReplyDelete
  13. hawawezi kuwa sawa wenye macho na vipofu , mola atakupa mwongozo ndugu yangu anonymus may 26 , 5:57

    ReplyDelete
  14. Mola hayuko pamoja na mwenye kukataa umoja. Haya ndio mafundisho ya dini yetu. Kila atakayejaribu kuvunja umoja laana itamuandama. Hujaona mifano basi? Wale wote waliotaka kuvunja umoja wetu mbio zao zimeishia wapi. Vile vikatuni vya muamsho vilivyojifanya vidume sasa viko wapi. Hii yote ni lana kwa mola wetu. Hebu someni dini muifahamu kwa undani. Aya moja ina maana zaidi ya 70 kwa mwenye kujua dini lakini. Umoja wowote wa wanaadamu ukiuvunja mola anakuanza hapa hapa duniani. Hebu fungeni safari muende mkoa wa kusini mkasome dini!

    ReplyDelete
    Replies
    1. sikubaliani na wewe kwamba Uamsho wanakataa umoja,bali Uamsho wanapinga DHULMA. Kuwekwa ndani kwao si mageni, haya na zaidi ya haya huwapata wale wote wanaopigania HAKI.Ijapokuwa umejinadi kwamba ni msomi nashangaa kutolijua hili.Wao watapata la kumjibu Mola wao watakapoulizwa mbele ya haki kuhusiana na DHULMA hii,sasa jiulize wewe utajibu nini?

      Delete
  15. Scotland wana referendum mwakani cc wazanzibari tutakuwa nayo lini ?

    Selenunda

    ReplyDelete
  16. Hayo alosema maalim, tuliyaona awamu ya2 yeye nakundilake wakasaliti leo iweje aje na fitina hizi sisi tulitaka 3 wao wakatuona baya bora mwalim,Jk nyerere sasa uwo nkataba hauji mtadanganyana sana hatutoi hata nyanda

    ReplyDelete
  17. Dhulma kubwa ni ile ya kukataa umoja ni ndio mahubiri yote ya Uamsho kuanzia kichwani mpaka miguuni mwao. Dhulma kubwa ni ile ya kuchoma mapira na kuharibu miundo mbinu inayotumiwa na waumini; dhulma kubwa ni ile kuigeuza siku ya ijumaa kuwa ya wasiwasi watu kuogopa kwenda kuswali kwa sababu ya Uamsho. Dhulma kubwa ni ile ya kuleta fitna kwenye nchi na hiyo ndio iliyokuwa kazi ya uamsho.

    Mkataa umoja ni mchawi! Mola yeye hawi pamoja na mkataa umoja. Mtahangaika tu hapa duniani na fitina zenu zisizokwisha. Hao mnaowafanya watume wenu kuwasalia kila siku yao tumeshayaona, hakuna zaidi ya u baguzi. Au mmesahau wakati hao walivyowagawa kati ya watu wa mtambwe na wapemba wengine hasa kutoka kusini? Enzi zao ni ntu ya ntambwe tu aliyekuwa ntu. Ubaguzi acheni hauna mwisho mwema.

    ReplyDelete
  18. semeni mnavyosema, muungano hautakiwi katika united islands of zanzibar ( UIZ) , na tena niwakumbushie, hata ukanda wa pwani wote wa tanganyika ni milki ya zanzibar , watanganyika hata bahari si yao kaangalieni historia mazuzute mlisoma , hapana shaka wale waliochangia kusema huu muungano umelaaniwa wana pointi ,

    ReplyDelete
  19. Sema usemavyo muungano huutáki wewe lakini sisi wengine tunautaka na utakuwepo

    ReplyDelete
  20. yakheeee , kama ni wakweli na waadilifu waambie basi hio serikali ya chama cha ma.. mabwa...mabwanyenye ( CCM ) waitishe kura ya maoni eehee , sasa yakheee wewe anonymus wa mwisho usiwapoteze raia wenzangu mayakhee na msimamo wetu wa kupinga muungano , wewe bila shaka ni shushushu eeheeheeee yakheeee, balaaaa!heeheeeee, haahaaahaaa , muungano umekwisha habari yake dah masikini muungano kwa heri eenheeeheeee , yakheeee , na kama unaogopa labda ukivunjika muungano utaambiwa urudi kwenu tanganyika basi usiwe na wasi yakheee , zanzibar na tanganyika zitakubaliana bila shaka kuwa raia wake wanaweza kuishi upande wowote bila wahka , ikiwa watu wa mataifa ya nje wanaishi znz , na tanganyika , nini kitazuia waznz au watngnyk kuishi popote yakheee

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.