Habari za Punde

Moto Small wanataka kurudisha hadhi


Kikosi cha timu ya Small Simba cha miaka ilee ambacho licha ya kuonesha kandanda la uhakika na kuvutia pia kilikuwa mwiba kwa timu za Simba na Yanga.

Kutoka kushoto waliokaa ni Idrissa Mohammed 'Killer' (marehemu) Omar Hassan (King), Issa (Alhadhir) Lambo, Mohammed Ukasha, Kapteni Fadhil, Ubwa Makame (Mzungu), Rashid Tall, Gharib Lato, Khamis Abofu.

Waliosimama kutoka kushoto Kocha msaidizi, Dr Mambi, Ridhaa Khamis, Rashid Khamis, ........., ........, Khamis Mpemba , Shaaban Mussa, ............ Kocha Abdulghani Msoma


Wapenzi na Wanachama wote waanzilishi wa iliyokuwa Klabu Maarufu ya mchezo wa soka hapa Zanzibar Timu ya kandanda ya Small Simba wanatarajiwa kukutana kesho asubuhi katika azma ya kutaka kuifufua tena Timu hiyo.
 
Kikao cha kutafakari mustakabali wa timu hiyo kinatazamiwa kuwa wazi kikikaribisha pia wadau wa klabu hiyo ambacho kitafanyika katika jengo la CCM la Jimbo la Kikwajuni liliopo hapo mnazi Mmoja Mjini Zanzibar majira ya saa 3.00 za asubuhi.
 
Akikaririwa na vyombo vya Habari Mmoja wa waanzilishi wa Klabu hiyo maarufu katika miaka ya 1980 na 90 Dr. Juma Mambi kwa niaba ya Katibu mteule wa Klabu hiyo Kassim Juma alisema mada tatu zitajadiliwa katika kikao hicho.


Dr. Mambi alizitaja mada hizo kuwa ni pamoja na Kujua mustakabali wa Small Simba, kufufua ari na hamasa za wapenzi wa Klabu hiyo pamoja na mengineyo yatakayojichomoza katika kikao hicho.
 
Dr. Mambi aliwaomba pia wana habari kushiriki katika kikao hicho lengo la kutafuta mbinu na njia ya kutaka kurejesha ari na hamasa ya mchezo wa soka ambao ulikuwa katika kiwango cha juu wakati timu hiyo ikiwa katika Nyanja za Kimichezo.
 
Timu ya Soka ya Small Simba iliwahi kushika ubingwa na soka wa daraja la kwanza hapa Zanzibar na kutoa upinzani mkali kwa timu za Yanga na Simba za Dar es salaam katika iliyokuwa mashindano ya klabu bingwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

1 comment:

  1. Duuu!..kaka kwakweli umenigusa sana! miaka ile nakumbuka nipo std. 5 J'mbe!

    Afadhali wafufue 'chama hilo' na mfadhili mkuu anaweza akawa huyo mdau wapili kushoto(waliochuchumaa) ana pesa za kutosha!

    Kwa sasa wafadhili wengi wa zamani, kama vile Hassan gharib, mabrouk lee n.k. aidha wameshachoka au wamesha tangilia mbele ya haki

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.