Ataka ZFA iache sumu ya kubaguana kimaeneo
Na Salum Vuai, Maelezo
MARA baada ya kuchukua fomu za kutaka kugombea nafasi ya urais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ibrahim Dharamsi Raza, amesema dhamira yake kuu ni kuiondeshea Zanzibar aibu inayotokana na kushuka hadhi kisoka.
Raza aliyechukua fomu hiyo jana katika ofisi za Kamati ya Uchaguzi ya ZFA iliyoko uwanja wa Amaan, alisema hafurahishwi na kuzorota kwa mchezo huo, hali inayowakimbiza mashabiki viwanjani.
Akijibu masuala ya waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu hiyo, Raza aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa mamlaka za michezo ikiwemo Makamu Mwenyekiti wa ZFA (1995-2000), alisema soka la Zanzibar limekosa uongozi makini na wenye uchungu wa kuliokoa.
"Inasikitisha kuona ni watu wachache sana wanaokwenda kuangalia mechi za ligi siku hizi, tafauti na zamani ambapo viwanja vya Amaan na Mao vilikuwa vikijaa na watu wakifurahika", alisema Raza.
Alisema iwapo atafanikiwa kushinda katika kinyang'anyiro hicho, anakusudia kushirikiana na viongozi wenzake na wadau wote wa soka nchini, kupanga mikakati madhubuti ili wanamichezo warejeshe imani kwa ZFA ambayo imepotea kutokana na uongozi usiojali maslahi ya umma na kuweka mbele ubinafsi.
Aidha, alisema lengo jengine ni kuhakikisha ZFA inaimarisha uhusiano wake na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na hivyo kudai mgao na haki zake zinazotokana na misaada ya FIFA kupitia mgongo wa TFF.
Mgombea huyo alisema, uongozi wake utakuwa wa pamoja kati ya Unguja na Pemba, akieleza kuwa bila ushirikiano kati ya pande hizo maendeleo yatakuwa ndoto.
Uchaguzi mdogo wa ZFA kujaza nafasi ya urais iliyoachwa wazi na Amani Ibrahim Makungu aliyejiuzulu mwishoni mwa mwezi Januari, unatarajiwa kufanyika Juni 8, mwaka huu katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani.
Kimsingi, Raza ni kiongozi hodarai katika mambo ya soka, tatizo lake ana mawazo ya Uwamsho kidogo.
ReplyDeleteHata ktk kampeni zake ameanza na kulalamikia mgao wa Z'bar ktk TFF na kuahidi kuwezesha Z'bar kujiunga na FIFA Jambo ambalo hataweza.
Anatakiwa atueleze ni namna gani atarudisha UPENZI wa soka Z'bar kama ilivyokua miaka ya 1980/90 pamoja na kuyashawishi makamuni kama PBZ na Z'tel kudhamini soka.
Miaka ile hatukua wanachama wa FIFA na mambo yalikua safi na ikiwezekana hata udhamini wa makampuni ya bia uruhusiwe.
Mnazuia matangazo ya ulevi lakini wenyewe mnakunywa na kuruhusu bia uingizwa visiwani sasa si bora wakapunguza hiyo faida wanayoipata kwa kudhamini michezo?
"KUTANGAZA BIA KHARAM, KUIINGIZA Z'BAR NA KUNYWA HALALI" 'Afatu'minuna bi'baadhil..kitabi, wa'takfuruuna..bi'baadhin'?
mdau namba 1 we chizi kweli kweli unaona sifa gani zanzibar kuruhusiwe matangazo ya pombe?
ReplyDeleteHayo aliyoyasema Raza ni madai ya walio wengi sio yake. FIFA, mgao wetu TFF nk
unakusudia nini mawazo ya kiuamsho we samaki nini!
Nikisema 'MAWAZO YA UWAMSHO' nakusudia kushughulikia mambo yasiyowezekana!
ReplyDeleteMimi sioni sifa yoyote kuruhusiwa kwa matangazo ya pombe na ikiwezekana nataka ipigwe marufuku hata kuingizwa hapa visiwani!
Lakini madam mnaruhusu iingizwe na kuuzwa kwa watalii na vijana wetu basi faida mnayoipata lazma mchangie katika michezo!
Kama vile wenye maduka ya pombe na mabaa wanavyolipa kodi na kuchangia ktk mishahara yetu, tunayolisha familia na kuchangia ktk miskiti yetu nk.!
Nadhani hiyo ayya ktk suratul baqara utakua imeielewa na haikuishia hapo huko mbele Allah anauliza"afala..taakiluun?
Na kwa taarifa yako madhara makubwa ya pombe yapo ktk kunywa nasio kutangaza.
Angalia ayya hizi:
Inna malkhamru, wal-maisir....................
La takrabu ssalaa in kuntum sukaara...........