Na Mwanaally Hamad,Dodoma
SERIKALI imesema itaendelea kuwachukulia hatua stahiki watumishi wote wanaokosa uadilifu katika utendaji wa kazi zao.
Akifungua warsha ya siku moja kwa Mameyaa, Wenyeviti wa Halmashaurri,Wenyeviti wa kamati za ukaguzi na wakaguzi wa ndani wa Manispaa,Wilaya na Miji mjini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia aliwataka watumishi hao kuwa makini,waadilifu na wawazi katika utekelezaji wa majukumu yaao kama yalivyoaainishwa katika sheria ya fedha za umma na waraka wa tawala za mikoa na serikali za mitaa wa mwaka 2007.
“Natambua kuwa si menejimenti zote za halmashauri zisizothamini umuhimu wa ukaguzi wa ndani,bali pia nina taarifaa baadhi ya waakaguzi wa ndani hawatekelezi majukumu yaao kikamilifu na hata uadilifu wao kutiliwa shaka,” alisema.
Aidha alisema kuna madai kuwa baadhi ya Menejimenti hazitoi uzito unao stahili kwa taarifaa zinazotolewa na wakaguzi wa ndani na hata wakati fulani kitengo cha ukaguzi wa ndaani hakipati mgaao wa fedhaa katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
“Natoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za serikali za mitaa, kuhakikisha kamati za ukaguzi zinatekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika kanuni ya sheria ya fedha za umma kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaondoa matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa madhumuni ya kuwaletea wananchi wetu maendeleo,”alisema.
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga alitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na idadi ndogo ya wakaguzi wa ndani ukilinganisha na mahitaji halisi katika Halmashauri za serikali za mitaa hasa baada ya kuanzishwa Halmashauri mpya na ongezeko mikoa mipya.
Mtonga alitaja changamoto nyingine kuwa baadhi ya sheria na kanuni kukinzana na sheria ya fedha sura 348 hasa zile za mamlaka za serikali za mitaa.
Nyingine ni baadhi ya maafisa masuhuli kutoshughulikia mapendekezo na ushauri unaotolewa na wakaguzi wa ndaani kwa lengo la kuboresha mifumo mbalimbali ya kiutendaji na hivyo kudhoofishaa juhuddi za serikali katika usimamizi na udhibiti wa rasilimali zake.
Warsha hiyo iliyoandaaliwa na kufadhiliwa na Wizara ya Fedha ina lengo la kuwaongezea uwezo wakaguzi wa ndani kufanya kazi zao kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ukaguzi wa ndani.
No comments:
Post a Comment