Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya SSB Said Salum Bakresa, akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, alipowasili katika viwanja vya Bandari ya Malindi kwa ajili ya Uzinduzi wa Jengo jipya la Abiria wanaosafiri kutumia Boti kwenda Dar na Pemba.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar BalozinSeif Ali Iddi, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya SSB Said Salum Bakresa alipowasili katika viwanja vya Bandari ya Zanzibar kuhudhuria sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Abiria wa boti zinazotowa huduma kwa Wananchi wa Dar na Pemba.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akimsalimiana na Meneja wa Kampuni ya Usafiri ya Hussein Said, wakati wa sherehe za kuzinduwa jengo jipya la Abiria Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akitembelea bandari ya Abiria wanaosafiri kwa boti akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya SSB, Said Salum Bakresa kuagalia sehemu za bandari hiyo iliojengwa upya kupitia mradi wa Kampuni ya Azam Marine.
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Bandari mpya ya abiria katika bandari ya Malindi huko Unguja leo. Kushoto ni Sheikh Said Salum Bakhresa.
|
|
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya SSB Said Salum Bakhresa, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar akiwa katika moja ya jengo hilo laabiria baada ya kulizinduwa kwa kutowa huduma ya Usafiri kwa Wananchi wa Zanzibar kwa safari za Dar na Pemba jengo hilo limetumia gharama ya shilingi bilioni moja hadi kukamilika kwa ujenzi wake. |
|
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamad (katikati) wakati alipotembelea sehemu ya kuegeshea meli ya mizigo. Kushoto ni Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na Sheikh Said Salum Bakhresa.
|
|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimkabidhi zawadi mfadhili wa Kampuni ya ujenzi wa Bandari mpya ya Abiria, Sheikh Said Salum Bakhresa, katika sherehe za ufunguzi wa Bandari mpya ya Abiria katika Bandari ya Malindi Zanzibar.
|
Anastahiki pongezi nyingi Bakhresa kwa uzalendo wake,na mapenzi yake kwa kuitupia macho angalau hiyo sehemu ya boti zake na nyengine huu ndio uzalendo na mapenzi ya mtu kwao,na hawa akina mwakijebe wamekuja kufanya nini?wakati ZNZ kuna waziri?au ndio mpaka tusimamiwe na bara?,wanja wa ndege mpaka leo umeshindikana kutengenzwa angalau uwe nao na sura mzuri hasa kwa wageni wanaotutembelea.
ReplyDeleteHuyu ni mtu ambae, serikali inatakiwa iwe naye karibu ili asaide mipango ya maendeleo.
ReplyDeleteHuyu kwa Z'bar ni kama BILLGATE kwa Marekani SMZ inatakiwa hata kufanya nae 'share' ktk baadhi ya biashara zake.
Vitegauchumi vyake kama vile vilivyopo nchini CONGO, UGANDA ZAMBIA na hata TZA bara SMZ ingeweza kujiongezea kipatao na kutafuta ajira za vijana.