Habari za Punde

DK Shein afutarisha Ikulu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akiwa na Viongozi wakati wa futari aliyowaalika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo usiku
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,(wa pili kulia) akiwa na Viongozi akina mama wakati wa Futari aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar leo usiku
  Baadhi ya Akina Mama walioalikwa katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,leo usiku katika viwanuja vya Ikulu Mjini Zanzibar
 Wananchi mbali mbali wa Manispaa ya Mji wa Unguja,waliohudhuria katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo usiku
Wananchi na Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi leo baada ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo usiku


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaaafu wa Zanzibar alhaj Dk.Amani Abeid Karume, baada ya futari aliyowaalika wananchi katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo usiku.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na wananchi katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo usiku,baada ya futari aliyowaalika katika mwezi huu wa Ramadhan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkwe Mama Mwanamwema Shein,wakiagana na wananchi katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo usiku,baada ya futari waliyowaalika katika mwezi huu wa Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

1 comment:

  1. Ndugu zangu hebu nisaidieni hii bajeti ya kufutarishana mwezi mzima inatoka wapi ktk serikali au jee?

    Lakuskitisha zaidi wengi kati ya waalikwa ni watu na uwezo wao wasikini wa ukweli hualikwa wachache tu kama kisingizio!

    Kwa ufupi zoezi Zima linakwenda kinyume na aliozo la M/Mungu la kufuturisha masikini wajane na mayatima

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.