Joseph Ngilisho, Arusha
NDEGE ya madaktari inayomilikiwa na Kanisa Katoliki imeanguka na kujeruhi vibaya abiria saba akiwemo rubani mmoja, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja mdogo wa ndege uliopi Merugwayi wilayani Longido mkoani Arusha.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Japhet Lusingu alisema ndege hiyo aina ya Cess yenye namba TN/4206 ilianguk muda mfupi baada ya kuruka umbali wa kilomita 120 kutoka uwanja huo.
Alisema ndege hiyo iliondoka jijini Arusha majira ya saa 2:00 asubuhi ikiwa na marubani wawili kuelekea wilayani Ngorongoro na ilianguka wakati ikijaribu kuruka kutoka Ngorongoro majira ya saa 8:00 mchana kurudi Arusha ikiwa na abiria watano.
Alisema ajali hiyo imesababishwa na hali mbaya ya hewa kutoka na upepo mkali uliokuwa ukivuma.
Alisema ndege hiyo ilianguka katika misitu kilomita 120 kutoka ulipo uwanja huo.
Hata hivyo, alisema baada ya kuanguka haikuungua na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya Selian kwa matibabu huku wengine hali zao zikiwa sio nzuri.
Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Nalepo Mamasita (38), Anna Laizer (21) NaninkoiLaizer (7), Banson Mukoya (28) Krizosto Malima (30) pamoja narubani JafferShakir ambaye alijeruhiwa vibaya.
Alisema majeruhi wameumia sehemu za uso, kichwa, mikono na sehemu nyengine za mwili.
Ndege hiyo inatumiwa na hospitali ya kanisa kuwasafirisha wagonjwa kutoka maeneo ya wafugaji.
No comments:
Post a Comment