Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Afungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Majaji na Mahakimu Afrika Mashariki.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa na Waheshimiwa Majaji wakisimama wakati ukipingwa wimbo wa Taifa katika Mkutano wa Ufunguzi wa Jumuiya ya Majaji na Mahakimu uliofanyika hoteli ya Zanzibar Beach.Mazizini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akifungua Mkutano wa 11 wa Jumuiya ya Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki, katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini Zanzibar.
 Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitowa maelezo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Jumuiya ya Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki,  






 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Othman Chande,akizungumzia Mkutano Mkuu wa 11 wa Jumuiya ya Majaji na Mahakimu, baada ya uzinduzi wamkutano huo uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
 Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman  Kakungu, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na Mkutano huo uliofanyika Zanzibar katika Hotel ya Zanzibar Beach Mazizini nje kidogo ya mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Waheshemiwa Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashariki baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo katika Ukumbi wa Hotel ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.