Habari za Punde

Uzinduzi wa Jengo la Madrasa Hidayat Islamia Kidoti na Rais wa Zanzibar Dkt. Shein.


Jengo jipya la Madrasatul Hidayat Islamia Kidoti Wilaya ya Kaskazini A Unguja lililojengwa kwa ajili ya kutoa Elimu ya Dini kwa Watoto wa Kijiji cha Kidoti .
Moja ya madarasa matano ya jengo hilo likiwa katika hali ya kupendeza na kuvutia  na Wanafunzi wa madrasa hiyo watapata mafunzo ya elimu ya dini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekliti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kuzindua Madrasa Hidayatul Islamia katika  Kijiji cha Kidoti Wilaya  ya Kaskazini A Unguja,(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe Juma Pembe
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika maandamano maalumo yalioandaliwa na madrasa hiyo wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo hilo jipya la Madrasatul Hidayat Islamiya Kidoti Unguja Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Mjenzi wa Jengo hilo akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, baada ya kulifungua jengo hilo akiwa na Makamo wa Pili wa Rais wa anzibar Balozi Seif Ali.wakimsikiliza mjenzi huo wakiwa ndani ya jengo hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekliti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na Wananchi na Wanafunzi wa madrasa Hidayatul Islamia ya Kidoti Wilaya ya Kaskazini A Unguja,Mkoa wa Kaskazini iliyojengwa kwa ufadhili wa wahisani mbali
mbali na Nguvu za Wananchi wenyewe
Mwanafunzi Ali Makame akisoma Quran wakati wa ufunguzi wa Madrasa yao huko Kidoti Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Mwanafunzi Shaban Mohammed akistowa Tafsiri ya Quran iliosomwa katika sherehe hizo za ufunguzi wa Madrasa yaoKidoti.
Mwanafunzi Rukia Machano akisoma risala kwa niaba ya Wanafunzi wezake wa Madrasa Hidayat Islamiya Kidoti katika sherehe za Uzinduzi wa jengo lao jipya.
Mwanafunzi Rukia Machano akimkabidhi Risala yao Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, baada ya kuisoma na kutowa maombi yao ya kusaidika kupatiwa Mafunzo kwa Walimu wao
Wanafunzi wa Madrasa Hidayat Islamia wakiwa katika viwanja vya madrasa yao wakishuhudia ufunguzi huo uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein,
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Mke wa Makamo wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman Iddi,na Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,na Naibu wa Wizara hiyo Haji Mwadini Makame Mwakilishi wa Nungwi (CUF) wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa  Madrasa Hidayatul Islamia katika kijiji cha Kidoti Wilaya ya Kaskazini A Unguja,uliofanyika leo kijijini hapo
Viongozi waliohudhuria katika ufunguzi wa Madrasa Hidayatul Islamia katika kijiji cha Kidoti Wilaya ya Kaskazini A Unguja,(kutoka kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Juma Haji Juma,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji
                          Wanafunzi wakifuatilia sherehe za uzinduzi wa Madrasa yao huko Kidoti.
Wananchi na Wazazi wa Wanafunzi wa madrasatul Hidayat Islamiya wakiwa katika viwanja vya madrasa hiyo wakifuatilia uzinduzi huo, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia baada ya kulizinduwa jengo hilo.
Wanafunzi wa Madrasatul Hidayat Islamiya Kidoti wakitowa Elimu ya kupitia onesho umuhumu wa kupata elimu ya Dini Watoto wakiwa na umri mdogo na manufaa yake,  wakati wa ufunguzi wa madrasa yao huko Kidoti.

2 comments:

  1. MashaAllah nijambo la kupingezana kwa wale wore wsliojaaliwa kufaniksha jambo hili ila tu lazima tubadilke na twende na wskati kwani si wakati tena wa wanafunzi kukaa chini na mwalimu kutumia chaki.Viongozi punguzeni ulafi muipeleke nchi kwenye karne ya 21.

    ReplyDelete
  2. Hii mibaibui ya kisomali na kanzu za kipakistani vyereje na utamaduni wetu. Kwanini watoto wetu wasivae kanga na wanaume kanzu na kofia.

    Raisi nae atafutiwe kazi ya kufanya kupoteza siku nzima na pesa zetu kwa kwenda kufungua chuo. Kwanini asiende mkuu wa mkoa tu.

    Inshallah chuo kizae maulamaa na maulamat kwa nchi yetu.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.