Habari za Punde

Mzee Mandela Atakumbukwa kwa Uongozi Wake.Kiongozi mashughuri wa Afrika ambaye leo hatunae tena ndugu yetu Nelson Mandela ametiachia miiko mingi ya uongozi ambayo kama viongozi wetu kuazia chini hadi juu watafuata nchi yetu itapata maendeleo ya haraka. Mandela alifuata mtindo wa uongozi wenye ukomo (self-limiting style of leadership). Pamoja na kupendwa kwake na wananchi alikaa kwenye kiti cha urais kwa miaka mitano tu. Wawakilishi wetu wanaotaka kuendelea kukaa kwenye majimbo yao kwa hali yoyote ile kwa miaka kadha wa kadha ni vyema kuanzia sasa wakajifunza kutoka kwa marehemu Mandela. Kung'ang'ania uwakilishi hata kama huna cha maana zaidi ya kuwagawa watu na kusambaza majungu ni dhambi kubwa ya uongozi. Wakati huu wa kukumbuka maisha aliyoishi Mandela ni cyema tukajifunza mambo muhimu aliyoyasimamia wakati wa uhai wake.

Hapa nanukuu makala yaliyoandikwa na Steven Friedman kutoka gazeti la Citizen la Afrika kusini tarehe 11 Disemba. "The most obvious evidence that he did not see himself as a messiah was hia insistence on serving only one term, which, ironically, did more to make this country safe for democracy than anything else he did"

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.