Habari za Punde

Ziara ya Kimasomo ya Wanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa Sheria Baraza la Wawakilishi

 

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mhe. Abubakar Khamis Bakar, akizungumza na Wanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Tunguu Zanzibar walipofanya ziara ya Kimasomo katika jengo la Baraza kujionea Uendeshaji wa Kikao cha Baraza. 
 Mbunge wa Bunge la Wanafunzo wa Chuo Kikuu cha Tunguu Masoud Salim akizungumza katika mkutano huo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Abubakar Khamis Bakar, walipofanya ziara ya kimasoma katika jengo la Baraza la Wawakilishi.


Wanafunzi wa mwaka wa Tatu wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Tunguu wakimsikiliza Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar Abubakar Khamis Bakar, walipofanya ziara ya kimasomo katika jengo la Baraza la Wawakilishi kuangalia uendeshwaji wa kikao hicho na kuona jinsi ya kuchangia Miswada ya Serekali inayowasilisha katika Kikao hicho.Kulikuwa kukijadiliwa Mswada wa Mazingira kwa Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu kutokana na uchimbaji wa vifusi katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa barabara Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.