Habari za Punde

CCM yaendelea kumnadi mgombea wake Kiembe Samaki


01
Mwenyekiti wa Mkoa wa magharibi kichama Yussuf Muh’d Yussuf  akimnadi mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mahmoud Thabit Kombo katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja. (Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).
02
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Mkoa wa magharibi kichama Yussuf Muh’d Yussuf (hayupo pichani) katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja.
03
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mahmoud Thabit Kombo akimpa maiki mwanawe Sukainnah Mahmoud Thabit awasalimie wanachama wa (CCM) katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki zilizofanyika Bustani ya Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi Unguja.
04
Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mahmoud Thabit Kombo akiwahutubia wananchi waliofika katika kampeni zake katika kiwanja cha Bustani ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja leo.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

1 comment:

  1. Assalaam alaykum
    Mh. Mahmoud mimi nakuamini sana kwa uwezo wako wa kulitete Jimbo la Kiembe samaki na watu wake kwa maslahi ya Zanzibar.
    Ila jambo moja halikunifurahisha, hiyo picha uliyopiga na mwanao wa kike, kama mzazi na kiongozi mtarajiwa picha hiyo inatoa ishara gani?? Ndio nchi yetu haina dini kama wanavyosema wanasiasa lakini watu tuna dini yetu(uislam), mila na silka zetu. Kupiga picha au kuwa na binti yako mbele ya hadhara ya watu katika hali aliyo (bila stara) inayostahiki kwa mtoto wa kike kiislam nadhani sio sahihi. Tutarajie nini kesho utapokuwa baraza la wawakilishi ukizungumzia suala la mmomonyoko wa maadili.
    Nadhani vazi alilovaa binti yako mbele halileti taswira njema kwa kiongozi mtarajiwa. Tujitahidi sisi viongozi katika kuchunga maadili ili tuwe kioo chema cha jamii tunayoiongoza. MOla atupe nguvu na imani ya kufuata maamrisho yake amiin.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.