Habari za Punde

Hapa na Pale katika maonyesho ya miaka 50 ya Mapinduzi

Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi akitembelea na kupata maelezo ya banda la Vyombo vya habari la  Zenj FM. 
Afisa wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO, akitowa maelezo kwa Rais Mtaaf wa Tanzania Mzee Alhajjj Ali Hassan Mwinyi alipotembelea banda hilo wakati wa ufungaji wa maonesho hayo ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika katika viwanja vya Beit Ras.
Ofisa wa Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu Zanzibar akionesha baadhi ya vifaa vinavyotumika na Idara ya Barabara katika kufanyia utafiti wa ujenzi wa barabara Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia Wananchi wakati akitembelea mabanda hayo baada ya kuhutubia kuyafunga maonesho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA Beit Ras.
Wananchi wakitembelea banda la PBZ na kupata maelezo ya huduma zinazopatikana katika Benki hiyo.
Mteja wa PBZ akitowa maoni yake kwa Maofisa wa PBZ wakati wa maonesho hayo ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. PBZ ilitowa huduma kwa wateja wake.

Maofisa wa Shirika la Posta wakiwa katika banda lao wakitowa huduma za kiposta kwa wateja waliofika katika maonesho hayo kwa huduma za kutuma barua na huduma nyengine za kiposta zilipatikana katika banda hilo.
Fundi wa Idara ya Karakana akitowa maelezo ya Ufundi unaotilewa kwa Wananchi wanaoleta magari yao katika karakana kuu ya Serekali Chumbuni.
Afisa wa Idara ya Kilimona Mifugo akitowa maelezo kwa Wananchi waliotembelea banda lao katika maonesho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
      Vifaa vinavyotumiwa na Shirika la Bandari Zanzibar katika kutowa huduma za baharini kuongoza Meli
Afisa wa Idara ya Uhamiaji Tanzania Tatu Burhan, akielezea matumizi ya Passport  na upatikanaji wake kwa Wananchi waliofika katika banda  lao kuona shughuli zinazofanywa na Uhamiaji Nchini katika kuhudumia wateja wao kupata Passport na Uraia.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.