Habari za Punde

Mkapa anguruma Pemba · Atakama maslahi ya walimu yaangaliwe

Na Haji Nassor, Pemba
RAIS mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Benjamin Mkapa, ametaka maslahi ya  waalimu yaangaliwe kwa kina ikiwemo suala la mishahara yao, ili wapate nafasi ya kufundisha vyema.
Alisema ni vyema kwa serikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi, kukaa chini na kutafuta njia mbadala ya kuwasiadia waalimu, hasa katika suala zima la kuwapandishia mishahara.
Alitoa kauli hiyo jana baada ya kukifungua chuo kipya ya ualimu cha Benjamini Mkapa  kilichopo Mchangamdogo wilaya ya Wete Pemba, ikiwa ni  shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema pasi na serikali zote mbili kuamua kwa makusudi kuitupia macho sekta hiyo, kamwe suala la maendeleo yasitarajiwe, kutokana na wafinyanzi hao kukosa uimara wa kazi zao.
Alisema sio busara hata kidogo kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kulisahau kundi hilo na kuendelea kuwa dhaifu na kisha kutafuta sababu ya wanafunzi kufeli makundi kwa makundi.

Alisema ni vyema waalimu wakaangalia kwa kina juu ya kuimarishiwa maslahi yao, hasa kutokana na kazi ngumu wanayoifanya ya kuwafinyanga viongozi wa taifa.
“Mwalimu Nyere alisema, ‘mwalimu wana nguvu’ ya kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo, endapoa wataangalia kwa kina juu ya kazi zao nzito wanazozifanya,” alisema.
Hata hivyo, alisema kusiwe na maswala mengi na kuhoji kwamba kwanini wakati wake hakuyatekeleza hayo, na kuutaka utawala uliopo sasa kujifunza kosa alilolifanya yeye.
“Mimi inawezekana hilo sikulifanya wakati wa utawala wangu, lakini isiwe sababu wa viongozi wa sasa na wao kuliacha badala yake walitekeleze kwa nguvu zote,” alisema.
Katika hatua nyengine, ameitaka jamii kuendelea kuwajengea heshima, urafiki na nidhamu waalimu kutokana na umuhimu wao katika taifa.
Alisema waalimu ndio wanaopewa mzigo mkubwa wa kuwalea watoto, tokea wakiwa wadogo hadi kufikia ngazi ya chuo, hivyo ni vyema wakajengewa nidhamu ya hali ya juu.
Akisoma risala ya waalimu na wanafunzi, Mwalimu Mkuu wa chuo hicho, Sadi Mohamed Seif, alisema pamoja na kumalizika kwa chuo hicho, lakini wanakabiliwa na ukosefu wa uzio.
Alisema uzuri na haiba ya jengo hilo, hautakuwa endelevu iwapo wizara ya elimu na wafadhili wengine, hawatoona umuhimu wa kujenga ukuta ambao utakuwa na uwezo wa kukihifadhi chuo hicho na eneo lake.
Aidha aliomba wizara, kuangalia uwezekano wa haraka wa kuwachimbia kisima katika eneo hilo, ili kukabiliana na uhaba wa huduma ya maji safi na salama unaoweza kujitokeza katika majengo ya chuo.
Nae Katibu Mkuu wizara ya elimu, Mwanaidi Salehe, alisema ujenzi wa chuo hicho, unajumuisha mradi wa kuimarisha elimu ya msingi, ambapo jumla ys dola 42 milioni za Marekani zimetumika ikiwa ni mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia.

Chuo hicho cha uwalimu cha Benjamini Mkapa ambacho kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 480 kwa wakati mmoja.

1 comment:

  1. Huyu leo ajifanya kuwa na hurum na walimu wa pemba wakati alipokuwa madarakani aliamuru, mahita na vikosi vyote vya ulinzi vipegena kubaka kulepema, bilikujali kuna walimu na wqanafunzi ,sasa anajidazi wema, waznz, hatusahau,aliopikosa tunzo ya m, ibrahim, alisema kama angeweza kurudi madarakani, .............wangemjua yeye nani?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.