Habari za Punde

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki kuzuru Zanzibar

TAARIFA YA ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UTURUKI
                   HON. AHMET  DOVUTOGLU TAREHE 31/5/2014.
 
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki Hon. Ahmet Dovutoglu atawasili Zanzibar  Siku ya Jumamosi tarehe 31/5/2014  kwa ziara ya siku moja.
 
Dovutoglo na ujumbe wake atawasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume saa 2.30 asubuhi na ataondoka siku ya Jumapili asubuhi.
 
Kwa taarifa hii unaombwa kushiriki katika ziara hiyo katika sehemu ambazo tutaruhusiwa kama ilivyo kawaida ya wageni  mashuhuri wanapokuwepo Zanzibar.
Ratiba  kamili tutaipata baadae ama Uwanja wa Ndege wakati wa mapokezi.
 
            IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.