Habari za Punde

Mama Mwanamwema Shein, Akabidhi Vifaa vya BrassBand ya Chipukizi na Kikundi cha Vijana Wapanda Pikipiki Pemba

Vijana wa Madungu Chakechake Pemba waonesha mchezo wa Sarakasi katika viwanja vya Skuli hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa vya Brassband bendi ya Chipukizi Pemba na kuzinduliwa Kikundi cha Wapanda Pikipiki. 
Mdau hao ni Vijana  wa Chipukizi Madungu Kisiwani Pembawakionesha jinsi wanavyocheza mchezo wa Judo, ikiwa ni burudani wakati wa kukabidhiwa Vifaa vya Brass Band Bendi ya Chipukizi Pemba na Mke  wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein,  

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akitowa nasaha zake kwa Vijana wa Chipukizi na Wananchi wa Wilaya ya Chakechake Pemba, katika hafla ya kukabidhi Vifaa vya Bendi ya Chipukizi Pemba na kuzinduwa Kikundi cha Vijana Wapanda Pikipiki Pemba, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Madungu Wilaya yaChakechake Pemba. 

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Vijana na kuwatambulisha Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM walounda Umuoja wao Kusaidia Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali katika Majimbo ya Zanzibar. Umoja huo tayari umeshatowa msaada kwa Majimbommbalimbali Kisiwanii Unguja na Pemba. Bila ya kuchangua jimbo.
Wazee wa CCM wa Wilaya Chakechake Pemba wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwahutubia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa Wanachipukizi wa Brassband. 
Vijana wapanda Pikipiki Kisiwani Pemba wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar,akiwazindulia Kikundi chao katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Madungu Wilaya ya Chakechake Pemba. 


Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Ndg. Shaka Hamdu Shaka, akihutubia wakati wa hfla hiyo ya kukabidhi Vifaa Band yaChipukizi Pemba na kuzinduliwaKikundi cha Vijana Wapanda Pikipiki Pemba katika viwanja vya Skuli ya Madungu Pemba. 
Mwenyekiti wa Vijana wa UVCCM Mkoa wa Kusini Pemba Ndg. Ali Juma Nassor, akiwahutubia Vijana wa Wilaya ya Chakechake na kutowa nasaha zake kwa Vijana wa CCM katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Madungu.  
Wazee wa CCM Wilaya ya Chakechake Pemba wakifuatilia hafla hiyo katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Madungu.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Madungu Pemba wakifuatilia na kumsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar, alipokuwa akihutubia katika hafla hiyo katika viwanja vya Skuli ya Madungu Sekondari Wilaya ya Chake Chake Pemba.

Vijana wa Chipukizin Wilaya ya Chakechake Pemba wakishuhudia makabidhiano ya Vifaa Vipya vya Bendi yao ya Chipukizi.katika viwanja vya skuli ya madungu.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.