Habari za Punde

Balozi Seif Amuandalia Tafrija Mgeni Wake Makamu wa Rais wa China

Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ukiendelea na mazungumzo yao na ujumbe wa China chini ya Makamu wa Rais wa Nchi hiyo Bwana Li Yuanchao hapo katika ukumbi wa Hoteli ya La Gema Nungwi. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kulia akimkabidhi Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao zawadi ya kasha kama kumbu kumbu ya ziara yake hapa Zanzibar mara baada ya kumaliza mazungumzo yao huko Nungwi.
Balozi Seif na Mgeni wake Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao  wakitoa nje ya ukumbi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyoshirikisha viongozi wa ngazi za juu wa pande zote mbili.
Bwana Christopher Mush Smith wa Hoteli ya La Gema akikata Keki Maalum yenye Bendera za Tanzania na China iliyoandaliwa na Hoteli hiyo kwa ajili ya Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Li Yuanchao aliyepo pembeni yake akiwa sambamba na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif na mgeni wake Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao wakifuatilia muziki laini wa kikunci cha taarabu asilia cha Akheri Zamani hakipo pichani kwenye tafrija yao hapo La Gema Nungwi.
Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao akipongeza na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika Hoteli ya La Gema Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Bwana Li Yuanchao upande wa kushoto alinyanyuka na kufurahia muziki murua uliokua ukiporomoshwa na Kikundi cha taadab asilia cha Akheri Zamani wakati wa tafrija yao kwenye Hoteli ya La Gema Nungwi. 
Ukumbi wa Hoteli ya La Gema Nungwi iliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ulisheheni vionja vya muziki wa Taarab asilia ya kikundi cha Akheri Zamani wakati wa tafrija maalum kwa ajili ya ugeni wa Serikali ya China uliooongozwa na Makamu wa Rais wa Nchi hiyo Bwana Li Yuanchao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.