Habari za Punde

Mwenge wa Uhuru wawasili Zanzibar

 Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Getrudi Mpaka akitoa salam za Mkoa huo kabla ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mjini Magharibi leo july 30.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis, makabidhiano hayo yamefanyika uwanja wa ndege mkongwe Kiembesamaki leo. (Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).
 Vijana wa Chipukizi wakiimba nyimbo ya Mwenge.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili Zanzibar.
 
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Hamza Ibrahim kutoka Mjini Magharibi na maaskari wakiukimbiza Mwenge.

 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima kwa ajili ya kuukimbiza katika Wilaya yake
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima akikimbiza Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini tayari kuanza ziara yake.(Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).
 

5 comments:

  1. Nnapita tu ntarudi baadae, kwani mwenge umo katika mambo ya muungano?

    ReplyDelete
  2. Swala lako gumu mdau

    ReplyDelete
  3. Anonymous1
    Mwenge haumo katika Mambo ya Muungano kwasababu huo Uhuru unaotokana na Mwenge huu ni Uhuru wa Tanganyika na Sio Uhuru wa Zanzibar.
    Lakini kama tunavojuwa sasa kwamba TANGANYIKA ndio TANZANIA ambayo Inaitawala Zanzibar na CCM Ndio Chama cha TANU kujibadilisha Jina na Kuifuta ASP ili sisi wengine wajinga tuone CCM imetokana na ASP na TANU....

    1. Kwa Ufupi Huu mwenge Unawapotezea muda watoto wetu wa Skuli kwani wanalazimishwa kwenda kupokea Mwenge kwa lazma..

    2. Mwenge huu pia unawatia hasara wafanyakazi wa SMZ ambao wanalazimishwa kulipa pesa za Mafuta ya Mwenge japokua hawataki na hela hiyo hukatwa direct kutoka kwenye Mishahara.. Infact hili suali la ukatwaji wa mishahara ya Wanyonge mimi nataka watu waiandikie article kwa wasemaji wakuu wa SUK ..

    Na kuna kipindi fulani sikumbuki alikua ni Raisi Babu Karume au Aboud Jumbe au Idrissa Abdul Wakil, hili Dude la Mwenge lilipigwa Marufuku Kuingia Zanzibar.. Na lilipoingizwa kwa nguvu na wale wahafidhuna wa wakati ule ulikua haupati watu wa kuukimbiza isipokua Makada ya CCM ambayop yamebatizwa na Kuamini kama Mwenge ni Suala la Muungano..

    Kazi kuabudu Moto na Kujipendekeza kwa Watanganyika UHURU gani huo Wazanzibari wanaoumurika wakati Uhuru wao Ulipinduliwa na hiyo TANU ..?

    ReplyDelete
  4. bado mnaabudu moto tu mpaka leo kweli bado kuna mijitu mijinga mijitu mizima na mijitumbo mnawavha familia zenu mnaingia barabarani mnakimbiza moto. kweli akili ni mali. teh teh teh .

    ReplyDelete
  5. Umeletwa kwa ajili ya vitambi noma hapo mbeleni.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.