Habari za Punde

Maalim Seif Ahudhuriwa Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Uturuki.

  1. Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan akijiandaa kuhutubia mkutano wa Dunia wa Uchumi, ambapo amezilaumu baadhi ya nchi za Magharibi, ikiwemo Marekani kutokana na sera zao nchini Irak na Syria.
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar wa Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na Waziri Mkuu wa Mali, Mhe. Moussa Mara (kulia) na viongozi wengine wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Uchumi wa Dunia, jijini Istanbul, Uturuki.
 Mhe. Maalim Seif akimsikiliza kijana wa miaka 22 ambaye amepewa heshima kubwa ya ubunifu wakati wa mijadala kwenye mkutano mkuu wa Uchumi wa Dunia (WEF) nchini Uturuki.
 Mh. Maalim Seif akibadilishana mawazo na Afisa katika Serikali ya Uturuki wakati wa mkutano wa Uchumi wa Dunia (WEF). 
Mhe.Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Italia, ambaye pia anahusika na Uturuki, James Msekela wakati wa mkutano mkuu.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif akitoka kwenye mkutano wa WEF. Kushoto kwake askari wa Uturuki akimhakikishia ulinzi.
  1. Wataalamu mbali mbali katika masuala ya Ubunifu na Ujasiri Amali, wakiwemo kutoka Israel, Marekani na Ujerumani waliofika katika mkutano wa WEF baada ya kuwasilisha mada zao. Mjadala wa mada hizo ulimhusisha Mhe. Maalim Seif.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.