Na Waandishi Wetu ZJMC.
Zanzibar.
Unaweza kustaajabu na
namna ya kipekee isiyomithilika, mandhari yake hutoa taaswira ya rangi ya
dhahabu kila jua linapozama, huku mvumo wa mawimbi ya maji yenye kuchanua,
yakigonga ukingoni mwa bahari ya hindi katika bustani ya Forodhani.
Bustani ya Forodhani ni
bustani ambayo inapatikana katika kisiwa cha Unguja maeneo ya mji mkongwe,
ambapo watu tofauti hufika kutokana na mandhari nzuri ya eneo hilo.
Uzuri wa mandhari hiyo
ni kuzungukwa na bandari kuu ya Zanzibar, pamoja na vivutio mbali mbali vya
watalii kama vile Beit-el-Ajaib, Ngome kongwe, jumba la kulelea watoto, pamoja
na makumbusho ya kasri, hali ambayo inapelekea mamia ya watu kuizuru kwa
nyakati tofauti.
Kwa upande wa shughuli
ambazo zinafanywa katika buastani ya Forodhani; ni pamoja na kupumzika, kustarehe,
matembezi pamoja na uuzaji wa biashara
mbali mbali za vyakula na vinywaji baridi vyenye asili ya
Zanzibar vyenye kusisimua, ni
miongoni mwa vivutio vinavyopatikana katika eneo hilo.
Licha ya kuwa na maeneo
ya kupumzika pia bustani ya Forodhani
ina sehemu tofauti zikiwemo sehemu ya kucheza watoto na kuogelea baharini.
Vile vile bustani ya forodhani ina sehemu
nzuri kwa ajili ya biashara ambayo hupatikana vyakula vya aina mbali mbali
vyenye mvuto wa kipekee kama vile Zanzibar pizza, chipsi kuku,urojo wa
kizanzibar, Vyengine ni mashelisheli ya kukaanga,mihogo,bila ya kusahau vyakula
yva baharini(sea foods) kama vile chaza,kaa, pweza na samaki wa aina mbali
mbali walioungwa kwa viungo maridhawa.
Kwa upande wa wafanya
biashara, makala haya ilibahatika kuongea na ndugu Said Ali Mwinyi ambaye ni muuza
vyakula vya baharini(sea food) na alieleza kuwa, anafurahishwa na kupata fursa
ya kufanya biashara katika eneo la bustani ya Forodhani kutokana na wageni
wengi kupendelea kununua vyakula vya aina hiyo.
Aidha aliendelea kusema
kiasi cha faida ni elfu thamanini huzipata ndani ya siku za jumamosi na
jumapili kutokana na wageni pamoja na wenyeji wengi hutembelea bustani hiyo
ndani ya siku hizo.
Hata hivyo bibi Raiyani
Khamis Ali, ambaye ni mkaazi wa Tunguu, hupendelea kuwepo siku ya jumamosi na
jumapili, ili aburudike na ladha tamu ya urojo wa kizanzibar na kuwatembeza
watoto wake ambao hufurahishwa zaidi na kuwepo utulivu, na mandhari ya bahari
pamoja na sehemu maalumu ya kufurahishia watoto.
Vijana wengi kutoka sehemu mbalimbali za ng`ambu na mjini hufika katika eneo hilo
kustarehe na kuogelea ukingoni mwa bustani hiyo.
“Unajua nini? nimekuja
hapa kwa ajili ya kupast time then nakumbukia mandhari ya home Nungwi,” hayo ni
maneno ya ndugu Hajji Ali Hajji, mkaazi wa Mwembe makumbi, wilaya ya Mjini akimaanisha kuvutika na mandhari ya bustani ya
Forodhani, baada ya kuhojiwa na waandishi wa makala haya.
Katika bustani hii,
wageni wanaopenda sana kutembelea ni
wataliano,ambpoi ni kutokana na kuwepo urahisi wa usafiri wa ndege ya moja kwa
moja kutoka Italy hadi Zanzibar.
Hivyo, wanapofika ndani
ya Zanzibar hupenda kuizuru bustani ya Forodhani kutokana na kuwepo kwa
mandhari nzuri na kupatikana vinywaji mbali mbali vyenye asili ya Zanzibar na
vyenye kusisimua.
Miongoni mwa vinywaji
wnavyopendelea zaidi wakiwa katika bustani hiyo ni juisi ya miwa ambayo ina
ladha nzuri ya asili na ni maarufu kwa wakaazi wa Zanzibar.
Sambamba na hayo bwana
Dickson Michael, raia wa Ujerumani, alisema hupendelea kuwepo ndani ya bustani
ya Forodhani nyakati za kuzama jua kwa lengo la kuiangalia na kutathmini
mabadiliko ya jua hilo wakati linapozama.
Bwana Bonifex Charles ambaye ni raia wa Italia
amesema anapenda kuwepo katika mandhari ya mwambao wa bahari hasa wakati wa jioni,
hivyo akiwa ndani ya mji wa Zanzibar hupendelae kuwepo katika bustani ya
Forodhani, kwani ni sehemu nzuri ya
mapumziko.
Akizungumza na
waandishi wa makala haya Bwana Captain
Rabbot ambaye ni raia wa Afrika Kusini aliyefika katika bustani hiyo, alisema
amefika hapo ili kustarehe na kuangalia tamaduni za watu wa aina mbalimbali.
Alisema anafurahishwa na bei za vyakula
vinavyouzwa hapo, kutokana na utofauti wa bei na nchi aliyotoka.
Sambamba na hayo
mamlaka ya mji mkongwe hujaribu kuifanya mpya bustani hiyo kila siku kwa
kuratibu mambo mbali mbali kama vile usafi wa mazingira, utunzaji wa nyasi,
pembea na mambo mbali mbali ya kufurahishia watoto, ambapo watoto wengi
hupedelea kufika hapo ili kufurahika na huduma hizo.
“Nikwambie kitu watu
ambao wamewahi kuja wakapata huduma nzuri pale, wameendelea kuwa ni mabalozi wazuri katika nchi zao,” alisema
ndugu Mussa Awesu Ameir, ambae ni mhandisi wa
mji mkongwe Zanzibar, wakati akizungumza na mmoja wa waandishi wa
makala haya.
Ndugu Mussa alisema
kwamba, bustani ya Forodhani hupendelewa kutembelewa na watalii na watu mbali
mbali nyakati za usiku mwepesi, ambapo huvutiwa na huduma zinazoendeswa chini
ya uongozi wa mamlaka ya mji mkongwe
Zanzibar.
Aidha ndugu Mussa
aliendelea kusema kuwa mara nyingi hupata fursa ya kuagiziwa vyakula mbali
mbali ambavyo vinauzwa ndani ya bustani ya Forodhani na kupelekwa nje ya nchi.
Hali hii husababishwa
na wageni wengi kutembelea na kujionea vyakula mbali mbali vinavyouzwa hapo na
kuvitangaza nchini kwao.
Bustani ya Forodhani
mwanzoni ilikuwa ipo katika usimamizi wa baraza la mji (manispaa) na baada ya
kufanyiwa marekebisho kwa kuboreshwa zaidi mnamo mwaka 2009,hapo ikawa chini ya
usimamizi wa mamalaka ya mji mkongwe kwa kuratibu shughuli zote zinazoendelea
hadi sasa.
Forodhani Park hakika
pahali mwanana pa kupumzika.tembele kujisijia raha.
PREPARED
BY; HAMAD SULEIMAN SHAABAN
SITI ALI SALIM
MWANAPILI KOMBO FASIHI
MWIABA KOMBO FASIHI
KHATIB KHAMIS ALI
ZENA ABDALLA ALI
QUESTION: TO WRITE FEATURE ABOUT FORODHANI PARK.
No comments:
Post a Comment