Habari za Punde

Maendeleo ya Msiba wa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Aliefariki Dunia mchana wa leo.

Marehemu Mhe Salmin Awadh Salmin Awadh. wakati wa uhai wake katika harakati za Siasa akiwa katika viwanja vya Komba wapya katika mkutano hadhara hivi karibuni.
Mwili wa marehemu Salmin Awadhi ukipakiwa gari tayari kwa taratibu za mazishi hapo kesho, katika makaburi ya makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja,  mwili wa marehemu unategemewa kuagwa kesho saa tano katika ukumbi wa baraza la wawakilishi Chukwani Unguja na kusaliwa katika Masjid Muhammad kwa mchina na kuzikwa Kijiji kwao Makunduchi Unguja  
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika nyumbani kwao marehemu mtaa wa mpendae kupata habari ya msiba huo. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndg Vuai Ali amesema marehemu alifika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui kwa kazi zake na kuhidhuria Kikao cha Sekreteli kilichofanyika asibuhi hofisini hapo , na kusema marehemu ametoka chumba cha mkutano na kwenda Afisi kwake ya Mnadhimu wa CCM Baraza la Wawakilishi, ndipo matatizo yalipojitokeza na kusema anasikia vibaya na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja kwa matibabu , kufika huko hali ilibandilika na kufariki dunia. Marehemu ameacha pigo kwa Chama na wananchi wa jimbo lake.
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Mahmoud Mussa , akiwa katika eneo la msiba akizungumza na ndugu na jamaa wa marehemu katika kupanga taratibu za msiba. 

Waheshimiwa Wabunge na Wawakilishi wakiwa na majonzi kwa msiba wa hafla wa Mwakilishi wa Magomeni na Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi wa CCMMarehemu Salmin Awadh Salmin.
Mhe Shamsi Vuai Nahodha na Mbunge wa Bububu Mhe Sururu kulia Mwakilishi Mstaafu Ali Shihata wakiwa katika viwanja vya msiba mpendae wakiwa na huzuni kwa kifo cha hafla cha mwakilishi wa jimbo la magomeni Zanzibar 
Waheshimiwa Wawakilishi Hanza Hassan na Ali Abdallah wakimfariji Mbunge wa Jimbo la Magomeni Hassan Chombo kwa msiba wa Mwakilishi wake kilichotokea hafla leo asubuhi 
Mhe Shamsi Vuai Nahodha akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika nyumbani kwa marehemu Salmin Awadh kufuatilia taratibu na mazishi ya marehemu na kutowa wasifa wake marehemu alikuwa jasiri na asiyependa kuonewa na alikuwa mtetezi katika vikao vya baraza la wawakilishi wakati wa kupitisha hoja 
Mbunge wa Jimbo la Magomeni Hassan Chombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kifo chake walionana muda mfupi kabla ya kumkuta mauti, amekuwa na majonzi na kustuka na msiba huo. ni pigo kwake.  wakiwa nyumbani kwa ndugu wa marehemu mpendae kunakofanyika maziko hayo hapo kesho saa saba baada ya sala ya Ijumaa masjid Muhammad kwa mchina na kuzikwa makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.

2 comments:

  1. Allah akubariki kwa kutupatia habari za nyumbani kwa wakati. Kwake tunatokea na kwake tutarejea.

    ReplyDelete
  2. Allah amsamehe makosa yake, Ameen

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.