Habari za Punde

Waziri Migiro kukabidhi nakala za katiba pendekezwa kwa asasi za kiraia na taasisi za kidini kesho

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, atakabidhi nakala za Katiba Inayopendekezwa kwa Wizara, Asasi za Kiraia, Taasisi za Kidini, Taasisi za Elimu, Vyama vya Watu Wenye Ulemavu na wadau wengine katika hafla fupi itakayofanyika kesho (Jumatatu, Machi 16, 2015) kuanzia saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. Mnakaribishwa tafadhali.

Itakumbukwa kuwa Serikali imeshagawa nakala za Katiba Inayopendekezwa katika mikoa na wilaya zote chini ya uratibu wa uongozi wa mikoa na wilaya. Kila kata imepelekewa nakala 300.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.