Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin
akisaini barua ya kampuni ya Zantel kwa ajili ya kuanza kulisaidia darasa la walemavu wa uoni wa shule ya msingi
Kisiwandui ambapo pia walikabidhi msaada wa jumla ya shilingi milioni 20.
Waanaotazama kutoka ulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kisiwandui, Bi Taifa
Ahmed, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Elimu, Bi Safia Ali, na mwisho kushoto ni
Shinuna Kassim, Mkurugenzi wa Mipango ya Biashara wa Zantel.
Mkurugenzi wa Elimu, Bi Safia Ali
akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa jumla ya shilingi milioni 20
kutoka kwa kampuni ya Zantel kwa ajili ya kununulia vifaa vya wanafunzi wa
ulemavu wa macho.
Mkurugenzi wa Zantel, Benoit Janin
akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa jumla ya shilingi milioni 20
kutoka kwa kampuni ya Zantel kwa ajili ya kununulia vifaa vya wanafunzi wa
ulemavu wa macho.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin
akimkabidhi, mwalimu mkuu, Bi Taifa Ahmed mfano wa hundi ya shilingi milioni 20
kwa ajili ya kununua vifaa vya wanafunzi wenye ulemavu wa uoni wa shule ya
msingi Kisiwandui.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin
akisaini barua ya kampuni ya Zantel kwa ajili ya kuanza kulisaidia darasa la walemavu wa uoni wa shule ya msingi
Kisiwandui ambapo pia walikabidhi msaada wa jumla ya shilingi milioni 20.
Waanaotazama kutoka ulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kisiwandui, Bi Taifa
Ahmed, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Elimu, Bi Safia Ali, na mwisho kushoto ni
Shinuna Kassim, Mkurugenzi wa Mipango ya Biashara wa Zantel.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin
akimkabidhi, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bi Taifa Ahmed barua inayoonyesha nia
ya kampuni ya Zantel kusaidia shule ya Kisiwandui. Anayetazama katikati ni Mkurugenzi
wa Elimu, Bi Safia Ali. Zantel pia walikabidhi shilingi milioni 20 kwa ajili ya
kununua vifaa vya walemavu wa uoni.
Mwanafunzi, Mbarouk Nassor akitoa
shukrani kwa kampuni ya Zantel baada ya kupokea msaada wa shilingi milioni 20 kwa
ajili ya kununua vifaa vya kuwasaidia kusoma.
Uongozi wa kampuni ya Zantel pamoja na
walimu na wanafunzi wa shule ya Kisiwandui katika picha ya pamoja baada ya
kupokea msaada wa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kununua vifaa vya walemavu
wa uoni wa shule hiyo.
Na Mwandishi Wetu.
Kampuni
ya simu ya Zantel leo imetoa msaada wa shilingi milioni 20 kwa wanafunzi wenye
ulemavu wa macho wa Shule ya Msingi Kisiwandui iliyopo Ugunja kwa ajili ya
kununua vifaa vitakavyo wasaidia wanafunzi hao wawapo shuleni.
Akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Zantel,
Benoit Janin alisema vifaa hivyo ni sehemu ya mkakati wa kampuni ya Zantel katika kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata elimu
bora bila kujali tofauti zao.
‘Wajibu
wetu kama wanajamii ni kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata msaada kama
ilivyo kwa watu wengine na pia kuweza kuwaanda kwa ajili ya kuweza kufikia malengo yao kama
walivyo kusudia’ alisema Benoit.
Vifaa
hivyo vipya ni sehemu ya jitihada za kampuni ya Zantel kwa ajili ya kushughulikia
mahitaji ya elimu kwa wanafunzi wenye walemavu ili kuhakikisha wanapata elimu bora
kama ilivyo kwa wanafunzi wasio na
ulemavu .
‘Kama
sehemu ya jamii tumedhamiria kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu kwa kuwapatia vifaa
wanavyovihitaji ili kuwasaidia kupata elimu bora, na kuanzia leo tutalichukua
darasa hili kuendelea kuwasaidia mahitaji mengine’ alisema Benoit.
Naye
Mkuu wa Shule hiyo, Bi Taifa Ahmed,
alitoa shukrani za dhati kwa Zantel kwa ukarimu wao na kusema kuwa msaada huo ni wa kipekee na
utarahisisha ufundishaji kwa wanafunzi hao, na hivyo kupelekea wanafunzi hao kupata
elimu bora kama ilivyo kwa wengine wasio na ulemavu.
‘Tunawashukuru
Zantel kwa kuziona changamoto tulizokuwa tunakabiliana nazo, na hakika kwa
msaada huu utatatusaidia katika kuwafundisha wanafunzi hawa na pia kuwawezesha kufikia malengo yao ' alisema Bi Taifa.
Katika hatua
nyingine, Mwalimu Taifa aliongeza kwa kusema kuwa wanafunzi wenye ulemavu ni
wanafunzi wa kawaida kama wanafunzi wasio na ulemavu hivyo wakiwezeshwa wanaweza
kushika nafasi yoyote katika jamii.
Shule
ya msingi Kisiwandui ilianzishwa mwaka 1991, na mpaka sasa wanafunzi 199 wamepitia
shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment