Mwandishi wa makala hii Muhamed Khamis akizungumza
na chifu wa kabila la kimasai katika kata ya idodi wilaya ya
Iringa vijijini Chif Lameck mtemisika.
University of Iringa (UoI)
0652729061
Tanzania ni miongoni nchi chake
katika bara la Africa iliojaaliwa kuwa na vivutio vingi vya
utalii.Tofauti na nchi nyengine nyingi za Africa na hata
katika bara la Africa iliojaaliwa kuwa na vivutio vingi vya
utalii.Tofauti na nchi nyengine nyingi za Africa na hata
dunia kwa jumla.miongoni mwa vivutio hivo vya utalii nchini
Tanzania ni mbuga za wanyama.
Katika mkoa wa Iringa ambao unapatikana nyanda za juu
kusini mwa Tanzania umejaliwa kuwa na mbuga ya
wanyama ‘Ruaha Nationa park’mbuga hii ipo magharibi mwa
Iringa katika kijiji cha tunga malenga kata ya Idodi kilimota
128 kutoka Iringa mjini.
Mbuga hii ni ya kipekee yenye wanyama wa kila aina na
adimu kupatikana kuonekana sehemu nyengine
ulimwenguni wanyama hao ni kama vile ‘kadu’ni aina ya
wanyama ambao kisura wameshabihiana sana na swala
lakini sio swala na ndio maana mwandishi wa makala hii
anasema mbuga hii ni ya kipekee, Kijografia mbuga hii ya
Ruaha imepakana na mikoa kadhaa ya Tanzania,miongoni
mwa mikoa hio ni singida,Dodoma,mbeya na ina ukubwa wa
kilomita za mraba 1300.
Wakaazi wa kijiji cha karibu na eneo
hili’tungamalenga’wameleza kusikitishwa kwao licha ya
uwepo wa kivutio kikubwa cha wageni lakini kwa upande
wao wanaeleza hawafaidiki na lolote lile kupitia mbuga hio.
Kwa nyakati tofauti wakizungumza na mwandishi wa makala
haya walisema uwepo wa mbuga hio kwao ni kama mzigo
kwani haina faida kwao,bali ni hasara inayotokana na
wanyama hao kwa vipando vyao mashambani.
Wamesema haina faida kwa sababu hakuna kijana hata
mmoja kutoka maeno hayo ambae ameajiriwa badala yake
huajiriwa zaidi wageni kutoka mikoa mengine jambo ambalo
linawalenga kuona uwepo wa mbuga hio ni kama mzigo na
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Bwana Silasi
mgeza alisema tokea kuanza uongozi wake takribani
mwaka mmoja sasa hajawahi kuskia wala kuona uwepo wa
ajira kwa vijana wake bali anachokijua yeye wanaoajiriwa
wote ni wageni wa eneo hilo.
Alisema hio ni changamoto kubwa kwa wanakijiji hicho
kwani matumaini yao waliamini uwepo wa mbuga hio
wangeweza kuajiriwa vijana wao lakini hali ni kinyume na
ndio maana wanasema mbuga hio ni mzigo kwao.
‘’licha ya uwepo wa kivutio hichi lakini hadi barabara hii ni
mbovu nadhani umeona ndugu mwandishi wakati unafunga
safari ya kuja kijijini hapa’’alieleza mwenyekiti huyo.
Licha ya tatizo hili la barabara lakini pia suala la elimu bado
kabisa miundombinu mibovu katika suala la elimu katika kijiji
hichi,wananchi waliamini uwepo wa secta hii ya utalii kwa
kiasi kikubwa ungesaidia secta hii ya elimu kwa kiasi
kikubwa ikiwa ni kujenga skuli ya kileo na kusaidia
kupatikana kwa walimu.
Rashid Salehe ni mwanafunzi aliehitimu kidato cha nne kwa
sasa anasubiri matokeo yake alisema anashangazwa hadi
leo hii shule yao ni mbovu huku kukiwa na uhaba mkubwa
wawalimu shuleni hapo,anaamini iwapo mbuga za wanyama
zingetumiwa vyema zingewasaidia wanafunzo mashuleni
kusoma katika mazingira bora.
Alieleza tayari amemaliza kidato cha nne lakini hana imani
kama anaweza kufaulu kutokana na ukosefu wawalimu
waliokuwa nao jambo ambalo linamkatisha matumaini
makubwa alikuwa nayo ya kufika chuo kikuu.
Aliamini kupitia waandishi wa habari kufichua
yanayowakabili kijiji kwao hwenda siku moja kijiji hicho
kikapiga hatua kimaendeleo kama vijiji vyengine Tanzania.
‘’Wakati mwengine natamani hata kuwalaumu wazazi wetu
ni kwanini walikubali uwepo wa hifadhi hii bila kutoa
masharti maalumu,angalia sasa watoto wao tunafeli kwa
kukosa walimu huku watoto wa wengine wanasoma vizuri
kupitia rasilimali zetu’’alieleza Rashid.
Tukizungumzia suala la afya katika kijiji hichi nalo pia
limeonekana kuwa mtihani mkubwa mwenyekiti wa serikali
ya kijiji cha Tungamalenga alinileza wana uhaba mkubwa
wa madaktari hospitalini hapo,jambo ambalo linawawia
vigumu sana kina mama wanaotaka kujifungua .
‘’Wake zetu wanalazimika kujifungulia Iringa mjini jambo
ambalo ni shida sana kutoka hapa mpaka Iringa mjini ni
karibu masaa manne,hali hii inaweza hata kupelekea kufariki
dunia wakati mwengine ukizingatia njia mbovu tulionayo
alinieleza mwenyekiti huyo.
Wahusika wakuu wa suala hili ni kina mama nao hawakuwa
kimya walipaza sauti zao wakati wakizungumza na
mwandishi wa makala hii ingawa hawakupenda kutajwa
majina yao kwa kuhofia kile kilichowakuta wenzao mwaka
jana ambapo walitoa taarifa kwa moja ya chombo cha habari
na wakapata matatizo makubwa kijijini hapo ingawa
hawakuwa tayari kueleza matatizo hayo.
Waliniambia changamoto kubwa wamekuwa wakizipata
wanapokwenda hospitali ya kijiji hicho ambacho dawa ni
kwa uchache sana lakini pia uhaba wa wauguzi hospitalini
hapo.
‘’Tunaiomba Serikali ichukue tatizo hili tukiwa kama
wananchi wa Tanzania ambao tunahitaji msaada wa
kutatuliwa changamoto zetu’’walieleza kina mama hao kwa
nyakati tofauti.
Wakazi wengi wa kijiji hichi cha tungamalenga ni wakulima
na wafugaji ingawa yapo makabila kadhaa yanayoishi
hapa,mwandishi wa makala hii alizungumza na mwenyeti wa
kijiji na kuelezwa makabila hayo ni wahehe,wangoni,wamasa
i na nk.
i na nk.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya kina mama ambao
wanajishughulisha na shughuli za kilimo walinieleza
wanatamani angalau kupatiwa nyezo za kilimo chao ili
watimize ndoto zao siku moja kuwa wakulima bora kama
walivo wengine.Walieleza wanatamani kuona angalau
uwongozi wa mbuga ya wanyama katika kijiji hicho
wanawapa kipaombele zaidi kutoka na shida walizonazo.
‘’Chakushangaza hawajali kabisa hata jitihada zetu na ndio
maana wanyama wao wanakuja hapa kila mda kuharibu
mazao yetu na wanajua kila kitu hatuna
lakuwafanya’’walieleza kina mama hao.
Jitihada za mwandishi wa makala hii zilikwenda mbali zaidi
kwa kufanikiwa kuonana na mmoja miongoni mwa walinzi
wa mbuga hio ambae hakupenda kutajwa jina lake kwenye
makala hii alisema ni kweli wananchi wa kijiji jirani hakuna
hata mmoja anaefanya kazi hapa(Tungamalenga).
Alisema wakuu wa sehemu hio wamekuwa wakitumia
kigenzo cha elimu katika ajira zao jambo ambalo ni
changamoto kubwa kwa wakaazi wa hapo ingawa wapo
wachache waliosoma lakini pia hawakuajiriwa.
Mlinzi huyo alieleza kuskitishwa kwake na utaratibu huo
ingawa yeye pia si miongoni mwa wananchi wa kijiji hicho
lakini alidai anaona uchugu zaidi kuona hakuna hata mtu
mmoja kutoka Tungamalenga alieajiriwa ingawa nafasi ni
nyingi zisizohitaji elimu.
‘’Zipo kazi tele hapa za kufanya kwa kutumia nguvu zaidi na
sio akili,aina hii ya kazi haihitaji elimu sijui ni kwanini uongozi
wa hapa unabaguwa katika ajira’’alieleza mlinzi huyo kwa
masikitiko.
Kuhusiana na suala la mapato yanayotokana na mbuga hio
mlinzi huyu alisema hana uhakika juu ya matumizi yake
sahihi ingawa anaamini ni lazima ubadhilifu uwepo
kutokana na hali halisi ilipo mbugani hapo na Tanzania kwa
ujumla.
Upande wa pili kwa wakaazi wa kijiji hichi ni kutoka katika
kabila la kimasaid ambapo mwanidishi wa makala hii
alikutana na kiongozi wa kabila hilo kuzungumzia uwepo wa
tatizo hili la ajira kwa vijana wa kijiji hichi.
Alisema hata wao ambao wana weledi mkubwa wa
wanyama wamekoseshwa ajira lakini hilo haliwaumizi zaidi
kinachowaumiza wao ni kuondolewa maeno wanayoishi kwa
madai kupewa wawekezaji huku wamamasai wakisahauliwa
kabisa.
‘Wametusahau kama sisi ni watanzaia kama walivowengine
pia tunahitaji haki kama wanayopewa wawekezaji,angalia
kundi hili la ngombe linakosa chakula sasa tumefukuzwa
kilichobaki ni kutuletea mgogoro na wakulima kwa
mashamba yao’’alieleza chifu lamek.
Alishauri Serikali kupitia wizara ya mali asili Tanzania
kuangalia upya suala la wawekezaji vyenginevyo linaweza
kuibuwa mgogoro mkubwa zaidi hapo badae lisipochukuliwa
hatua suala hili.
Jicho la Serikali limekuwa likiangaza zaidi kuhusiana na
suala la ujangiri kwa wanyama pori huku wakisahau uwepo
wa hali hio unatokana na tatizo la wananchi wenyewe
kutokufaidika na hifadhi zao na ndio maana wamekuwa na
maamuzi yasiosahihi kwa taifa huku wakiamini ndio njia
peke ya kujinufaisha kupitia mali zao.
Tanzania iwapo itatumia vyema rasilimali zake zilizonazo ni
wazi kabisa tutafika mbali kimaendeleo ikiwa tutakubali
rasilimali hizi ziwafaidishe watanzaia wenyewe na sio
wageni au wachache huku tukiwasahau wananchi wanaoishi
karibu na rasilimali zao.
Naamini suala la ujangiri na mabaya yote kwa rasilimali zetu
yataondola iwapo watanzania watakuwa miongoni mwa
wanaofaidia kinyume na hivi sasa ambapo watanzania
wamekuwa njia ya kuwafaidisha wachache miongoni mwao.
No comments:
Post a Comment