Habari za Punde

Ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya Milele Chakechake Pemba

VIONGOZI mbali mbali wa serikali kisiwani Pemba, kutoka kushoto ni Sheha wa sheria wa Mfikiwa akizushuhudia ufunguzi wa jengo la ofisi ya Milele Zanzibar Foundation huko Mfikiwa Chake Chake Pemba.
JENGO la Ofisi ya Milele Zanzibar Foundation Kisiwani Pemba, lililofunguliwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid, huko Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Msoma utenzi Halima Juma akighani Utenzi wake wakati wa ufunguzi wa jengo la la ofisi ya Milele Zanzibar Foundation, huko Mfikiwa Wilaya ya Chake Chake Pemba.
Mratibu wa Ofisi ya Milele Zanzibar Foundation kisiwani Pemba, Abdalla Said (Dula dii) akisoma risala ya milale wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo huko mfikiwa Chake Chake Pemba


Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Salum Kitwana Sururu, akitoa shukurani za Wizara kwa uongozi wa Milele Zanzibar Foundation, wakati wa uzinduzi wa ofisi huko Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Viongozi mbali mbali wa Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation, wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdall wakati alipokuwa kizungumza na wananchi, wakati wa ufunguzi wa Jengo la ofisi huko Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Mwakilishi wa FAWE Kisiwani Pemba mwalim Hija Hamad Issa, akitoa salamu za FAWE kwa viongozi wa Milele Zanzibar Foundation wakati wa uzinduzi wa jingo la ofisi hiyo huko Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Mwakilishi wa Milele Zanzibar Foundation bibi Sharifa Hamid Seif, akitoa salamu zake kwa wananchi, Viongozi wa Serikali wakati wa ufunguzi wa jingo la ofisi ya milale huko Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akikata utepe kuashiria kuzundua jingo la ofisi ya taasisi ya Milele Zanzibar Foundation, huko Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akikata keki kuashiria kutimiza miaka miwili tokea kuasisiwa kwa taasisi ya Milele Zanzibar Faoundation, wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi huko Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akibadilishana mawazo na mwanzilishi wa milele Zanzibar foundation bibi Sharifa Hamid Seif, kabla ya kuzindua ofisi ya Milele huko Mfikiwa Chake Chake Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla katikati, akiwa na watendaji wa Taasisi ya Milele Zanzibar Faoundation pamoja na viongozi wa serikali wakati wa picha ya Pamoja, mara baada ya kuzindua ofisi ta taasisi hiyo huko Mfikiwa Chake Cahke Pemba .
(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.