Habari za Punde

Wapenzi wa Kundemba wanapoishangiria Timu yao ikicheza

Timu ya Kundemba ambayo ipo katika daraja la pili Wilaya ya mjini Unguja, ni mojawapo katika timu chache zilizo madaraja ya chini lakini huvuta hisia za wapenzi wengi wa mpira wa miguu kiasi cha kuchangamsha Uwanja na watazamaji kwa vionjo lakini pia kuwatia mori wachezaji wa Kundemba kwamba jukwaani wana mchezaji No 12 anawefuatilia kwa karibu na kuwapa sapoti.

Hapa Kundemba ilikuwa ikicheza na Timu ya Gulioni, na wapenzi walitinga Uwanjani na Dufu kuwaunga mkono wachezaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.