Habari za Punde

TANZANIA NA UENYEKITI WA KUNDI LA NCHI ZA AFRIKA KATIKA UMOJA WA MATAIFA

Na MwandishiMaalum, New York                       
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa,   ni Mwenyekiti wa Kundi la  Nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa March. 

Miongoni mwa majukumu ya Mwenyekiti wa Mwenzi ni pamoja na kuitisha , kuratibu na kuendesha mikutano inayowahusisha Wawakilishi wa Kudumu kutoka Nchi 53 wanaoziwakilisha Nchi zao katika Umoja wa Mataifa.

Mwenyekiti wa mwezi,  pamoja na kuratibu na kuendesha mikutano yenye ajenda mbali mbali pia anawajibika katika kuwasilisha kauli ya nchi za Afrika kupitia ama utoaji wa hotuba au  mawasilianona Wakuu wa Idara mbali mbali ndani ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa, akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pale  inapolazimu.

Pichani ni baadhi ya Matukio yaliyotokea mwishoni wa wiki wakati wa Mkutano wa Wawakilishi hao wa Nchi za Afrika chini ya uenyekiti wa Tanzania, ambapo walipokea taarifa mbali mbali kutoka kwa watendaji wa Umoja wa Mataifa pamoja na taarifa kutoka kwa Muungano wa Wakuu wa Idara za Takwimu kutoka Afrika waliokuwa wakishiriki katika Mkutano wa 48 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.  Mkurugenzi  Mkuu wa Ofisi  ya Taifa ya Takwimu, Dr. Albina Chuwa  akitoaa raarifa  fupi kwa niaba ya Wakurungezi  Wakuu wa Idara za Takwimu kutoka  Nchi za Afrika kuhusu maazimio na mapendekezo yao  kuhusu viashiria vya ajenda  ya Maendeleo Endelevu.  Kulia kwa Balozi Tuvako Manongi ambaye  Tanzania ni Mwenyekiti wa Mwezi wa  nchi za Kundi la Afrika ( African  Group) Ni Mtakwimu Mkuu kutoka Ivory Coast.
 Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi wa Idara ya Siasa ya Umoja wa Mataifa, Bw. Taye-Brook Zerihoun  naye akiwasilisha taarifa yake kwa Wawakilishi wa Kudumu wa Nchi za Afrika, ambapo pamoja na mambo mengine aliwaomba wawakilishi hao kuunga mkono pendekezo la  Idara yake la kupatiwa fedha ambazo wanataka kuzitumia katika eneo la uratibu na usimamia wa majadiliano  kuhudu dhana  nzima ya uzuiaji wa machafuko ( mediation and  prevention ) pamoja na kuongeza ajira.
 Mkurugenzi Mkuu wa UN-Women Phumzile Mlabo Ngcuka  akiwaeleza Mabalozi kuhusu mkutano wa 68 wa Kamishini  Juu ya Hali ya  Wanawake  utakaoza siku ya Jumatatu hapa  Makao  Makuu ya Umoja wa Mataifa,Mada  kuu ya Mkutano  wa mwaka huu ambao huwakusanya mamia ya viongozi wanawake kutoka mataifa yote duniani  ni  Uwezezaji wa Wanawake kupitia utekelezaji wa  Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( aganda 2030) Kushoto wa  Balozi  Manongi ni  Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataita,  Balozi Antonio Tete
 Sehemu ya Mabalozi na Maafisa  kutoka   nchi Wanachamawa Umoja wa Afrika  wakifuatilia mkutano.
 Balozi Tuvako Manongi akimkabidhi zawadi ya kumuanga  kwa niaba ya  Mabalozi wenzie  aliyekuwa  Mwakilishi wa  Kudumu wa  Liberia katika Umoja wa Mataifa, Balozi Marjon V. Kamara ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje  wa Liberia. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.