Habari za Punde

Serikali Haitamuonea Muhali Yoyote Atakayehusika na Uingizaji wa Dawa za Kelevya Nchini.

Na. Miza Kona Maelezo – Zanzibar.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga mikakati maalum ya kuzifilisi gari zitazokamatwa au kuhusika uingizaji wa dawa za kulevya  kwa lengo la kudhibiti  uingizaji,  usambazaji na utumiaji wa dawa hizo nchini .

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed  huko Mnara wa kumbukumbu Kisonge katika Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Matumizi ya Dawa za Kulevya Duniani amesema serikali haitamuonea muhali yoyote atakae husika na uingizaji wa biashara ya dawa za kulevya kwa lengo la kutomeza janga hilo linathiri jamii na kupoteza nguvu ya Taifa.

Amesema wafanyabiasha wa bidhaa hiyo hawalitakii mema Taifa kwani wao ni wahujumu  wanaorejesha maendeleo ya nchini wanawaumiza vijana na watoto na kupoteza nguvu kazi ya Taifa hivyo wanahitaji kufichuliwa kwa nguvu bila ya kuwaonea muhali.

Ameeleza kuwa tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya linamtoa mtu katika hadhi yake ya ubinadamu kwa kutengwa na jamii na kumsababishia madhara makubwa ikiwemo maradhi ya Ini, Figo, Ukimwi na Ugonjwa wa akili pamoja na kupoteza viungo muhimu vya mwili.


Aidha Waziri Aboud amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa siasa wanawatumia vibaya madaraka yao kwa maslahi yao binafsi kuwatumia vijana kinyume na sheria jambo ambalo linachangia vijana hao kijiingiza katika vikundi viovu na hatimae kujiingiza katika utumiaji wa dawa hizo kwa kuwapotezea malengo na kuiathiri jamii.

Waziri huyo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu milioni 200 Duniani  wameathitika na utumiaji wa dawa za Kulevya ambapo Zanzibar watu 10000 wameathirika na utumiaji wa dawa hizo kati ya 3200 wanatumia niia ya kujidunga sindano .

Hata hivyo Waziri huyo amewata wazee na walezi kuwalea vyema watoto wao kwa kuwafunza maaadili mema ili kuweza kujiepusha na kujiingiza katika vikundi viovu sambamba na kuwapokea walioathirika na utumiaji wa dawa za kulevya kwa kuwajali , kuwakubali, kuwasidiana pamoja na kuwapa ushauri  kwa lengo la kuwaondolea matatizo yao ili wasirejee tena katika janga hilo.

Nae Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Moh’d Mahmoud ameitaka jamii kushirikiana kwa pamoja  ili kuweza kuwadhiti janga hilo kupitia njia zote zinatumika kupitishia dawa hizo kwa kukata minyororo iliomo katika sehemu husika kwa lengo la kutokomeza uingizaji wa bidhaa haramu nchini.  

Akitoa taarifa ya Jeshi la Polisi Mngwali Ussi amesema jumla ya kesi 79  zimeripotiwa  kati ya kesi saba zinahusiana na dawa za kulevya ambazo zinaendelea mahakani na kesi 72 za makosa tofauti ambazo ziko chini ya upelele wa polisi.

Wakitoa ushahidi vijana waliopata nafuu wameionya jamii wasiwaachie watoto wao kukaa katika vikundi na kujiepusha na marafiki waovu  kwani ndio kishawishi kikubwa  kinachopelekea watoto hao kujiingiza katika dimbwi la dawa hizo

Siku ya Kupambana na Usafirishaji na Utumiaji wa Dawa za Kulevya Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 26 Juni ambapo Ujumbe wa Mwaka huu Tuwajali, Tuwasikilize  Watoto na Vijana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.