Habari za Punde

Naibu Waziri wa Afya atembelea vituo vya afya Wilaya ya Kaskazini B unguja

 Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman wapili Kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkunga wa Kituo cha Afya cha Kiwengwa Khadija  Ali Juma Wakati alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya Afya Kaskazini  B Unguja.

 Naibu Waziri wa Afya  Harusi Saidi Suleiman katikati akiangalia shimo la Uchomwaji Taka linalotumiwa na Kituo cha Afya cha Kiwengwa baada ya kufanya ziara katika vituo vya Afya Kaskazini  B Unguja .kushoto ni  Mkunga wa Kituo cha Afya  Kiwengwa Khadija  Ali Juma.
 Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akisaini Kitabu cha Wageni mara baada alipofika katika kituo cha Afya cha Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini B Unguja
 Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman wakwanza kulia akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Bumbwini Misufini  Dk, KHamisi akitoa maelezo ya  Kumkaribisha  mara baada ya kufika katika Kituo hicho Mkoa wa Kaskazini B Unguja.
 Mhudumu wa Afya  wa Kijiji  cha Bumbwini Misufini Riziki Kiongwe Debe akitoa maelezo kuhusu changamoto zinazo wakabili kwa Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman (Hayupo pichani )mara baada ya kufika katika Kituo kilichopo kijijini hapo Mkoa wa Kaskazini B Unguja .

Naibu Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akifafanua jambo alipokutana na Wauguzi wa kituo cha Afya cha Bumbwini Misufini Mkoa wa Kaskazini B Unguja.kulia ni Afisa wa Afya Wilaya Mosi Kali Makame.
PICHA NA MIZA OTHMAN-MAELEZO ZANZIBAR.


Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar .

 Naibu Waziri wa Afya Harusi   Said Suleiman amesema hapendelei kuona  wauguzi wanatumbuliwa  majipu kutokana na uzembe wao  lakini hayuko tayari kutumbuliwa yeye kwa ajili yao

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akifanya ziara ya kutembelea vituo mbali mbali vya Afya Wilaya ya Kaskazini B Unguja  vikiwemo Kituo cha Kiwengwa  na Kituo cha Bubwini Misufini kutaka kuona changamoto zinazopo vituo hapo.

Alisema kuna baadhi ya wauguzi huwafanyia dharau wagonjwa au wajawazito wakati wa kujifungua jambo ambalo halipaswi kuona linafanyika, kitu ambacho kinaweza kuwapeleka pabaya na kutumbuliwa majibu.

“Sitoona  vizuri kuona mfanyakazi anatumbuliwa jipu kwa ajili ya uzembe wake na pia siko tayari kutumbuliwa mimi kwa ajili yake “Alisema Harusi .

Aidha alisema kwamba  wauguzi wawetayari kukamilisha majukumu yao ya kikazi na waache lugha chafu ambazo zitawasumbuwa wagonjwa na kuonekana kuwa wao wakorofu katika kutoa huduma .

Hata hivyo Naibu Waziri alieleza kuwa wauguzi waelewe kuwa awamu iliopo hivi sasa ni awamu ya uwajibikaji  na ufatiliaji na ni rahisi mawasiliano kufika kwa haraka na kuweza kuharibu  malengo ya baadae hivyo wasiwe tayari  kuchokozwa wakachokozeka.

Nae Muuguzi wa kituo cha afya cha Kiwengwa  Khadija Ali Juma alieleza matatizo mbali mbali ambayo wanakabiliana nayo kituoni hapo ikiwemo kutokuwa na uzio katika eneo hilo, wananchi kuchafua katika kwa makusudi katika maeneo ya vyoo pamoja na kufanya maskani katika kituo hicho .

Aidha alisema kutokuwa na friji katika kituo hicho kunachagia usumbufu mkubwa wa kuhifadhia dawa za chanjo za mama na watoto ambazo zinahitajika kuhifadhiwa katika sehemu yenye ubaridi ili zisiharibike .

Alisema ushirikiano mdogo uliopo baina ya kituo cha afya na kamati ya sheha hawaufurahikii wauguzi ,kwani sheha wa sehemu hiyo haonyeshi  ushirikiano mzuri na wauguzi waliopo katika kituo hicho .

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya alitembelea katika Kituo cha Afya cha Bumbuni Misufini ambacho kilitokezea matatizo ya kutofahamiana kati ya Wauguzi wa serikali na Wakunga wa Jadi .


aliwataka wauguzi ambao ni waajiriwa wa serikali kutoa mashirikiano ya pamoja na  wakunga wa jadi ili kuepusha tofauti miongoni mwao na kuweza kutatua changamoto ambazo zitaweza kujitokeza  kwa wazazi .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.