Habari za Punde

WAJUMBE wa Bodi ya Mfuko wa barabara Zanzibar ziarani Pemba kukagua miradi

 MATENGENEZO makubwa yanayoendelea kufanywa katika barabara ya Bahanasa-Mtambwe, ili kuzuwia barabara hiyo kuliwa na maji ya mvua wakati mvua itakaponyesha katika eneo hilo, kazi hiyo ikifanywa na kampuni ya MECCO.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 WAJUMBE wa Bodi ya Mfuko wa barabara Zanzibar, wakijadiliana jambo mara baada ya kuikagua matengenezo yanayoendelea kufanywa na kampuni ya MECCO katika barabara ya Bahanasa-Mtambwe, barabara hiyo nimiongoni mwa barabara tano za mkoa wa kaskazini Pemba, zilizojengwa na kampuni ya H-Yang.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 INJINIA Mkaazi wa Wizara ya Miundombinu Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, Khamis Massoud akimueleza kitu Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa barabara Zanzibar, Mwalimu Haji Ameir wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi kukagua barabara ya Bahanasa-Mtambwe inavyoendelea na ukarabati wake.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 MAFUNDI wakiendelea na kazi ya ujenzi wa njia maalumu za kupitia maji, katika matengenezo yanayoendelea ya barabra ya Bahanasa-Mtambwe kupitia kampuni ya MECCO, kama wanavyoonekana katika picha.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 GARI la Wizara ya Miundombinu Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, likiwa katika mtambo maalumu wa kupikia lami Vitongoji, likipakia lami hiyo na kwenda kuwekwa katika barabara ya Mgagadu-Kiwani inayoendelea na kazi ya uwekaji wa lami kwa sasa.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 MTAMBO wa Kubanjia Kokoto wa Wizara ya Miundombinu Mawasiliano na Usafirishaji Kisiwani Pemba, ukiwa katika kazi za ubanjaji wa kokoto huko Vitongoji Wilaya ya Chake Chake Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 MTAMBO wa Kupikia Lami Vitongoji Wilaya ya Chake Chake Pemba, ambao kwa sasa umeshachakaa na kuhatarisha maisha ya wafanyakazi katika mtambo huo, pichani mtambo huo ukiwa katika kazi zake za upikaji wa lami.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)


WAJUMBE wa Bodi ya Mfuko wa barabara Zanzibar wakiangalia kazi ya uwekaji wa lami katika barabara ya Mgagadu-Kiwani, inavyoendelea wakati wa ziara yao ya siku mbili kisiwani Pemba, kutembelea barabara mbali mbali kisiwani hapa.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
GARI maalumu ya kuwekea lami Kisiwani Pemba, ambapo kwa sasa gari hiyo imeshachoka huku ufanyaji wake wa kazi ukiwalazimu mafundi kuwa na spana mkonini, likiw akatika kazi zake za uwekaji wa lami katika barabara ya Mgagadu-Kiwani.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.