WAZIRI wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline Cyrus Castico, akizungumza na
wafanyakazi wa Idara ya Ustawi wa Jamii Pemba, juu ya kuimaliza haraka nyumba
ya wazee Limbani Wilaya ya Wete, wakati alipoitembelea nyumba hiyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MMOJA wa Mafundi wanaofanya ukarabati katika nyumba
ya wazee limbani Wilaya ya Wete, akiwa katika harakati zake za kikazi, pichani
fundi huyo akichukuwa jipsamu kwa kwenda kupaka katika moja ya sehemu za nyumba
hiyo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline Cyrus Castico, akitoa agizo kwa Idara
ya uwezeshaji kuijengea uzio nyumba ya wazee limbani Wete.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline Cyrus Castico, akikagua mipaka ya
nyumba ya wazee limbani Wilaya ya Wete, wakati wa ziara yake ya siku mbili
Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
BANDA la kufungia asali la kikundi cha Pemba Clove
Honey lililoko Kinyasini Wilaya ya Wete, likiwa na mizinga ya nyuki kwa ajili
ya kutega asali.(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.)
WAZIRI wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana,
Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe:Maudline Cyrus Castico, akikagua shamba ya
misan flower la kiku ndi cha Pemba Clove Honey lililoko Kinyasini Wilaya ya
Wete.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MITI ya Misan Flower ikiwa imenawiri katika shamba
linalomilikiwa na kikundi cha Pemba Clove Honey kilichopo Wete.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
No comments:
Post a Comment