Habari za Punde

Hospitali ya Abdalla Mzee karibu kumalizika ujenzi wake

 JENGO jipya la Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, ambalo tayari imeshafikia hatua za mwisho na wakati wowote wajenzi kutoka kampuni ya Jiangsu Provincial Construction Company LTD ya nchini China watalikabidhi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed, akipokea maelezo kutoka kwa Afisa Uendeshaji Tiba Pemba dk: Ali Mbarawa (mwenye shati la vyumba), wakati Waziri huyo alipoitembelea Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed (mwenye suti nyeusi), akiwa na uongozi wa wizara ya Afya, wakati akikagua ujenzi wa hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).


MASHINE ya CITI  ‘scanner’ ambayo ipo kwenye hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, ambayo kabla ya hospitali hiyo, kujengwa upya haikuwepo hospitalini hapo  (Picha na Haji Nassor, Pemba)
 Vitanda vyake vya kisasa,
 VITANDA maalumu kwa ajili ya wagonjwa wanaohitajia uangalizi maalum ICU, vilivyomo hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
PICHA ya pamoja baina ya uongozi wa wizara ya Afya na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe: Khalid Salum Mohamed mwenye suti nyeusi, mara baada ya kuikagua hospitali mpya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, (Picha na Haji Nasor, Pemba).    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.