Habari za Punde

Mkutano wa Mazingira Pemba.

Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na Mazingira Juma Bakari Alawi, akifungu mkutano wa matokeo ya Tathmini za athari za Maizngira kwa wadau kutoka taasisi mbali Kisiwani Pemba.

Washiriki wa mkutano wa kuongeza Tathmini za athari za mazingira Zanzibar, wakimsikiliza kwa makini mgeni Rasmi katika Mkutano huo wakati alipokuwa akifungua mkutano huo uliofanyika nje ya mji wa Chake Chake Pemba
Mtaalamu kutoka Kamisheni ya Tathmini za Kimazingira nchini Netherlands, Ineke Steinhauer akiwasilisha mada katika mkutano huo wa Tathmini ya athari za Mazingira Zanzibar uliowashirikisha wadau kutoka taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi zinazojihusisha na masuala ya mazingira
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar Sheha Mjaja Juma, akiwasilisha mada ya matokeo ya Tathmini za athari za Mazingira kwa wadau wanaohusika na masuala ya kimazingira Kisiwani Pemba, mkutano huo uliofanyika nje ya mji wa Chake Chake
Mwakilishi wa Wizara ya Miundombinu Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, Ali Mohamed akichangia katika mkutano huo wa tathmini za kimazingira. 
Mwezeshaji wa mafunzo ya matokeo ya Tathmini za athari za Mazingira Dk Aboud S Jumbe, akiwasilisha mada katika mkutano huo uliowakutanisha wadau kutoka taasisi mbali mbali za Serikali na binafsi zinazojihusisha na masuala ya Mazingira
Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na Mazingira Juma Bakari Alawi, akijadiliana jambo wataalamu mbali mbali juu ya mkutano wa kutathmini athari za Mazingira Kisiwani Pemba
Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na Mazingira Juma Bakari Alawi, akijadiliana jambo wataalamu mbali mbali juu ya mkutano wa kutathmini athari za Mazingira Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.