Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakiwa katika mstari tayari kumpa mkono Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Augustine Mahiga mara baada ya kumalia hotuba yake
Balozi wa Tanzania nchi Marekani Wilson Masilingi akimpa mkono wa pongezi Waziri Mahiga baada kumaliza hotuba yake mbele ya wajumbe wa mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Dk. Tausi Kida Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF naye akimpongeza Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mhe. Anna Lupembe Mbunge wa Viti Maalum (CCM) naye akimpongeza Mhe, Waziri kwa hotuba yake iliyopokelewa vizuri.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Dkt. Augustine Mahiga anayemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akiwasilisha mbele ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo ( hawapo pichani) vipaumbele vya Tanzania.
Na
Mwandishi Maalum, New York
Tanzania
imeeleza kwamba juhudi za serikali ya awamu ya
Tano za kukabiliana na vitendo
vya rushwa hazitaweza kufanikiwa kama
havita ungwa mkono na jumuiya ya
kimataita.
Ni kwa sababu hiyo, Tanzania, inazitaka nchi
zilizoendelea kuwawajibisha wawekezaji wao na makampuni yao ili yalipe kodi.
Hayo
yameelezwa jana jumatatu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Dkt. Agustine
Mahiga ( Mb) wakati alipolihutubia Baraza Kuu la 71 la Umoja wa Mataifa na
kutumia fursa hiyo kuelezea vipaumbele
vya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Mahinga akafafanua kwamba, lengo namba
kumi na sita la maendeleo endelevu
linatambua kuwa, rushwa inakandamiza
juhudi za kumbana na umaskini na usawa wa jinsia, inazuia
fursa na inakuwa na kama kodi kwa familia maskini pale wanapotafuta haki.
Ni
katika muktadha huo, akasema, serikali ya
Tanzania imeamua kuanzisha vita dhidi ya rushwa kwa kuhuisha uwazi, uwajibikani na usahihi katika utoaji wa huduma kwenye taasisi za umma.
Akasisitiza
kwamba serikali imeweka misingi mizuri
ya uwajibikaji inayomtaka mtumishi wa
umma kutambua kwamba wajibu wake wa
kwanza ni kutoa huduma bora na kwa
wakati kwa umma.
“Juhudi hizi za serikali za kupambana na rushwa hazitaweza kuzaa matunda bila ya kuungwa mkono wa jumuiya ya kimataifa. Nchi zilizoendelea zinatakiwa kuwawajibisha wawekezaji wao pamoja na makampuni yao ili waweze kulipa kodi stahiki.” Akaeleza zaidi Waziri Mahinga
Na kuongeza. “Ni lazima wawe tayari kurudisha
mali na fedha zilizoibwa kutoka nchi
zinazoendelea na kuzificha katika nchi zao ili mali na fedha hizo ziweze kusaidia maendeleo yetu”.
Kuhusu
fursa za jinsia na uwezeshwaji wa wanawake,
Waziri Mahinga ameelezea juhudi
mbalimbali ambazo zimefanywa na serikali katika
kuwawezesha wawanake ikiwamo
kushika ngazi za juu za maamuzi kuanzia serikali kuu hadi bunge na uwezeshwaji wa kiuchumi.
katika
kudhibitisha kuwa Tanzania inazingatia
usawa wa jinsia katika uteuzi wa ngazi
mbalimbali za maamuzi, Waziri
Mahinga ameeleza kwamba kwa mara ya
kwanza wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Rais John Pombe Magufuli alimchangua mwanamke kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
“Uteuzi huu
unathibitisha nia ya nchi yangu ya kuona wanawake wengi zaidi wanakuwa katika nafasi za ngazi za juu za
maamuzi. Na ajenda hii ya uwezeshwaji wa wanawake wa Tanzania sasa inamilikiwa
na wanawake wenyewe” akasisitiza Waziri
Kwa upande wa vijana, Kiongozi huyu wa Ujumbe
wa Tanzania ambaye amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema.
Vijana ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote lile, siyo tu
kwamba ni viongozi wa kesho lakini pia ni viongozi wa sasa.
Akatahadharisha
kwamba kwa kutowapa kiupaumbele vijana ni kujitafutia matatizo makubwa kutokana na kile alichosema ni
rahisi kurubuniwa na makundi ambayo ni
hatari kwa ustawi wa jamii na taifa .
“
Kutoka na kwamba idadi ya vijana ni
kubwa, serikali inachukua hatua mbalimbali
za kuliwezesha kundi hili la jamii
ambalo ni muhimu katika utekelezaji wa ajenda 2030. Na ili vijana
waweze kutekeleza jukumu hilo serikali imeanzisha mfuko wa maendeleo wa vijana mfuko ambao hadi mwezi March mwaka huu
jumla ya shiling 1.6 bilioni
zilipelekwa kwa vikundi 284 ya vijana”.
Kuhusu elimu,
eneo ambalo ni kipaumbele kingine cha Tanzania, Waziri ameeleza kuwa upatikanaji wa elimu jumuishi na ya viwango ndicho kipaumbele cha serikali
kwa kuwa Serikali inaamini kuwa, elimu ni ni nyenzo muhimu kwa maendeleo endelevu
Akafafanua kwamba
serikali inatekeleza bila kuchoka
kuhakikisha kwamba watoto wote wa kike
na wa kiume wanapata elimu bure kuanzia
shule ya msingi hadi sekondari. Pamoja na kutoka elimu
bure, serikali imeboresha mitaala yake kwa kuzingatia mahitaji ya karne ya 21.
“Alipoingia
madarakani, Mhe. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania alitangaza kwamba kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari itakuwa bure. Serikali imetenga zaidi ya shilingi 263 bilioni ili kuhakikisha
elimu inakuwa bure kwa wote.
Vipaumbele
vingine vya Tanzania ambavyo Mhe. Waziri
amevianisha katika hotuba yake ni pamoja na mikakati ambayo serikali imejiwekea katika utekelezaji wa mkataba wa mabadiliano
ya tabia nchi ( Paris Agreement),
utekelezaji wa malengo ya
maendeleo endelevu ( agenda 2030), mapambano dhidi ya dawa haramu za kulevya, na
kukabiliana na ugaidi ambao amesema ni
tatizo ambalo linaendelea kukua na kuwa tishio hata kwa nchi za Afrika Mashariki.
Kwa
upande wa utekelezaji wa agenda 2030,
Waziri amesema agenda hiyo imeanishwa
katika mipango ya kitaifa ya
miaka mitano ya maendeleo
kwa pande zote za muungano. Hata
hivyo amesema kuwa Tanzania imebaini kwamba haitaweza kukamilisha
kwa wakati agenda 2030 pasipo
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Kuhusu migogoro inayoendelea katika nchi za Burundi
na Sudani ya Kusini, Waziri Mahiga
amezitaka pande zote zinazopingana nchi
Burundi kutambua kwamba majadiliano ambayo ni jumuishi kwa pande zote
ndiyo njia sahihi ya kutatua matatizo ya
nchi yao.
Kwa
upande wa Sudani ya Kusini, Waziri amesema Tanzania inaungana na nchi nyingine kulaani matukio ya hivi
karibuni ya kujirudia kwa machafuko nchini humo.
Na
kuongeza, Tanzania ambaye ni Mwenye -Kiti wa sasa wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, iliitisha kikao
kisicho cha kawaida ili kuzungumzia hali
ya kisiasa ya Burundi na Sudani ya Kusini. “
Tunatumaini kwamba nchi zote
mbili zitaweka maslahi ya wananchi wao mbele ili kumaliza
machafuko”.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki pia aligusia kuhusu marekebisho ya mfumo wa Baraza
Usalama la Umoja wa Mataifa, ili
liwe jumuishi.
Kwa
upande wa Uchaguzi wa Katibu Mkuu, Waziri
amesema, Tanzania inaunga mkono hoja ya kuendelea kuheshimu utaratibu wa kupokezana nafasi
ya Katibu Mkuu kwa kuzingatia mzugunko
wa kijiographia.
No comments:
Post a Comment